RP-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing RP-Department of Kiswahili and African Languages by Author "Masika, Mark Elphas"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Polisemi ambazo Zimeundwa Kutokana na Sitiari na Metonimu katika Kiswahili(EANSO, 2024-02) Masika, Mark Elphas; Mwita, Leonard ChachaMakala haya imechunguza polisemi ambazo zimeundwa kutokana na sitiari na metonimu katika Kiswahili. Kimsingi, polisemi ni leksimu moja yenye maana nyingi ambazo zinahusiana kwa njia moja au nyingine. Pia polisemi huundwa kwa njia zingine kwa mfano, ukopaji, mabadiliko katika matumizi ya neno, na ufasiri mpya wa homonimu. Nadharia ya semantiki tambuzi ilitumiwa katika uchambuzi wa data ya utafiti huu. Nadharia hii ni sehemu ya nadharia ya Isimu Tambuzi ambayo ina misingi yake katika saikolojia tambuzi . Data ya makala haya ilikusanywa maktabani. Maneno ambayo ni polisemi na yameundwa kwa sitiari na metonimu kwenye Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2018) yalikusanywa. Mbinu ya usampulishaji wa kimaksudi ilitumika katika uteuzi wa sampuli. Kutokana na data ya utafiti huu, imebainika kuwa kuna baadhi ya polisemi zilizojitokeza ndani ya homonimu. Kwa mfano, tata1 na chuo1. Pia, utafiti huu umebaini kuwa polisemi nyingi huundwa kisitiari ikilinganishwa na metonimu. Makala haya inapendekeza kwamba tafiti zingine zaidi zinaweza kufanywa kuhusu namna mbinu zingine za lugha kama vile chuku, methali, nahau na tashibihi zinaweza kuchangia katika Isimu.