BC-Department of Kiswahili and African Languages
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing BC-Department of Kiswahili and African Languages by Author "Okora, Mogondo Erickson"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
Item Usawiri Wa Waathiriwa wa Ghasia Za Kisiasa na Kijamii Katika Riwaya Teule za Kiswahili(Kenyatta University, 2023-11) Okora, Mogondo EricksonUtafiti huu ulichunguza usawiri wa waathiriwa wa ghasia za kisiasa na kijamii katika riwaya za Chozi la Heri (Matei, 2014) na Kufa Kuzikana (Walibora, 2003). Riwaya hizi ziliteuliwa kutumia mbinu ya usampulishaji nasibu kwani zinadhihirisha matukio na wahusika wa ghasia za kisiasa na kijamii na zilitosheleza mahitaji ya uhakiki huu. Lengo la kwanza la uhakiki huu lilikuwa kubainisha waathiriwa wa ghasia za kisiasa na kijamii katika riwaya teule. Lengo la pili lilikuwa kuchunguza namna waathiriwa wa ghasia za kisiasa na kijamii walivyosawiriwa katika riwaya teule. Lengo la tatu lilikuwa kutathmini maudhui yaliyokuzwa na kuendelezwa na wahusika wa ghasia za kisiasa na kijamii katika riwaya teule. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhalisia. Mihimili ya nadharia ya nadharia ya uhalisia ilifaa utafiti huu katika kukusanya, kuchanganua na kuwasilisha matokeo kulingana na malengo ya utafiti. Utafiti huu ulifanyika maktabani ambapo data ilikusanywa kupitia usomaji wa riwaya teule kisha kuchanganuliwa na kuwasilishwa kwa mtindo wa maelezo. Utafiti huu umegawika katika sura tano; sura ya kwanza inahusu utangulizi wa utafiti ambapo tuliangalia usuli wa mada, malengo ya utafiti, suala la utafiti, na maswali ya utafiti. Aidha sura hii ilionyesha upeo na mipaka, yaliyoandikwa kuhusu mada, sababu za kuchagua mada, mbinu na nadharia ya utafiti. Sura ya pili inahusu ubainishaji wa wahusika wa ghasia za kisiasa na kijamii katika riwaya za Chozi la Heri na Kufa Kuzikana. Sura ya tatu ilichunguza namna wahusika wa ghasia za kisiasa na kijamii walivyosawiriwa katika riwaya teule. Sura ya nne inahusu kutathmini maudhui yaliyokuzwa na kuendelezwa na wahusika wa ghasia za kisiasa na kijamii katika riwaya teule. Sura ya tano inahusu muhtasari wa tasnifu nzima, matokeo, mapendekezo, mchango wa utafiti na changamoto za utafiti.