Usawini wa wahusika makahaba katika riwaya za Said Ahmed Mohammed

dc.contributor.authorAugustine, Muindi
dc.date.accessioned2012-05-17T13:06:26Z
dc.date.available2012-05-17T13:06:26Z
dc.date.issued2012-05-17
dc.descriptionThe PL 8704.M6 A8en_US
dc.description.abstractUtafiti wetu unahusu suala la ukahaba katika riwaya nne za Said Ahmed Mohammed. Tunahakiki usawiri wa wahusika makahaba kwa madhumuni ya kubainisha sababu za kuwepo kwa ukahaba katika jamii. Aidha, tunatalii namna ambavyo mwandishi anawabadilisha wahusika wake kutoka kwa maisha ya ukahaba na kama mabadililo hayo yanatoa suluhisho halisi kwa jamii ya makahaba. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa ndipo tunapojadili tasnifu kwa jumla, mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti wetu, upeo wa utafiti wetu. Vile vile, tunajadili baadhi ya kazi nyingine zilizowahi kuandikwa na ambazo kwa namna fulani, zinahusiana na utafiti wetu. Aidha, tutasema machache kuhusu nadharia tunayotumia katika utafiti wetu. Kisha tutatazama sababu za kuchagua mada hii na njia tutakazofuata katika kutafiti juu ya mada yetu. Katika sura ya pili na ambayo ndiyo nguzo ya utafiti, tunaelezea dhana na nadharia za ukahaba. Dhana na nadharia hizi zinatusaidia katika kubainisha vigezo mbalimbali vinavyotambulisha kahaba katika jamii. Tunafikia upeo wa utafiti wetu katika sura ya tatu na nne. Katika sura ya tatu, tunanuia kubainisha sababu mbalimbali ambazo zimewavuta baadhi ya wahusika katika maisha ya ukaha ba. Sura ya nne, tunajadili namna ambavyo mwandishi anawaondoa wahusika wake kutoka kwa maisha hayo. Sura ya tano ni ya hitimisho. Tunatoa muhtasari wa kazi tuliyoifanya. Kisha, tunatathmini kama tumefikia malengo ya utafiti wetu. Mwisho tunatoa marejeleo ya utafiti wetu.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/4662
dc.language.isoenen_US
dc.subjectKiswahili literatureen_US
dc.titleUsawini wa wahusika makahaba katika riwaya za Said Ahmed Mohammeden_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Augustine, Muindi.pdf
Size:
86.24 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Abstract
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
2.68 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: