Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kama nyenzo ya kukuza na kuendeleza Kiswahili’ in Lugha na Maswala Ibuka

dc.contributor.authorOsore, Miriam
dc.date.accessioned2023-11-22T16:31:29Z
dc.date.available2023-11-22T16:31:29Z
dc.date.issued2018
dc.descriptionBook Chapteren_US
dc.description.abstractMatumizi ya Kiswahili yametanuka kimaeneo kutoka pwani na maeneo ya Bara Hindi na kuendelea kutumika katika nchi nyingine barani Afrika na mabara mengineyo. Kiswahili sasa kinatumika katika nchi ya Kongo, Afrika Kusini, Rwanda, Burundi, Gabon, Marekani, Ujerumani, Bara la Ulaya, Uchina na kwingineko. Kiswahili kinatambulika miongoni mwa lugha kuu za kimataifa kama vile Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kihispaniola, na hata Kireno. Kati ya lugha za Kiafrika kama Hausa na Kilingala, Kiswahili ndiyo lugha ambayo imeenea kwa kasi na kuvuka mipaka ya bara la Afrika hadi kwingineko ulimwenguni. Awali, wamisionari walipofika Afrika Mashariki, walijifunza Kiswahili. Waliporejea kwao, walianzisha mafunzo ya Kiswahili kwa wale ambao walinuia kuzuru Afrika Mashariki kwa shughuli mbalimbali kama biashara, dini na utawala. Wataalamu wengi wa bara la Ulaya, walijitolea kufanya utafiti na kuandika vitabu kuhusu Kiswahili. Kwa mfano, Askofu Steere, Whiteley, Ashton na Krapf. Waliandika vitabu kama vile Handbook of Swahili Language (1870) cha Steere na Swahili Dictionary (1850) .cha Krapf. Uandishi wa vitabu hivi ni miongoni mwa hatua za mwanzo za kukiendeleza Kiswahili. Huko Marekani, Wamarekani wenye asili ya Kiafrika na Wazungu wamekuwa wakijifunza Kiswahili kama mojawapo ya masomo katika vyuo vikuu. Kwa Wamarekani weusi, hatua hii ni kama kielelezo cha urithi wa utamaduni wao. Barani Afrika, Kiswahili kinatumiwa kuleta utangamano kati ya jamii mbalimbali. 123 Kiswahili kimeteuliwa kama lugha mojawapo iliyo rasmi ya Umoja wa Afrika (VA). Lugha nyingine ni Kiingereza, Kifaransa, Kiispaniola, Kireno na Kiarabu. Aidha, Kiswahili ndiyo lugha rasmi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika. Katika kiwango hiki, Kiswahili ni lugha ya kimataifa. Kiswahili kimepanda hadi ngazi ya kimataifa kwa sababu mbalimbali. Kwa mujibu wa Mbaabu (1979) baadhi ya sababu hizo ni kwamba Kiswahili ni lugha ambayo haina mihemko ya kisiasa; inakubali mabadiliko ya istilahi mpya na unyambuaji wa maneno. Aidha, Kiswahili hakina vikwazo vya kimazingira; kina maandishi, historia na fasihi yake (Chiraghdin na Mnyampala, 1977).en_US
dc.identifier.citationMiriam Osore (2018): ‘Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kama nyenzo ya kukuza na kuendeleza Kiswahili’ in Lugha na Maswala Ibuka’, edited by Kandagor M. Obuchi, S. M. and Mwanakombo, N. M., Nairobi, Chama cha Kiswahili cha Taifa, pp 123 – 135. ISBN: 978-9978-5058-56.en_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/27178
dc.language.isootheren_US
dc.publisherChama cha Kiswahili cha Taifaen_US
dc.titleTeknolojia ya Habari na Mawasiliano kama nyenzo ya kukuza na kuendeleza Kiswahili’ in Lugha na Maswala Ibukaen_US
dc.typeBook chapteren_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kama Nyenzo ya Kukuza na Kueneza Kiswahili.pdf
Size:
5.54 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text Book Chapter
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: