Unyanyasaji dhidi ya wanaume katika fasihi andishi ya Kiswahili

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011-12-21
Authors
Gitau, Elizabeth Nyambura
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia maudhui ya unyanyasaji dhidi ya wanaume kama unavyodhihirika katika kazi teule za fasihi andishi ya Kiswahili. Katika kuendeleza kazi hii, mtafti ameteua kazi za waandishi wa kike na wa kiume katika tanzu za tamthilia na riwaya. Kazi zilizohakikiwa ni riwaya mbili, moja ya Z. Burhani (1981), Mali ya Maskini na ya Ken Walibora (1996), Siku Njema. Tamthilia zilizochambulia zilikuwa mbili, moja ya Wole Soyinka (1974), Masaibu ya Ndugu Jero, (Tafsiri na A. S. Yahya), pamoja na ya Ari Katini Mwachofi (1987), Mama Ee. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ile ya umuundo-utekelezi. Nadharia hii hueleza kuwa jamii ni mfumo unaochangiwa na vipengele vyake vyote ili kuleta muumano na utangamano. Nadharia hii husisitiza juu ya utekelezaji wa majukumu na wanajamii ili waendelee kuwa vipengele muhimu vya jamii. Tasnifu hii imegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia mada ya utafiti, malengo ya utafti na pia sababu za kuchagua mada hii. Sura hii vile vile, imegusia udurusu wa maandishi yanayohusu mada ya utafiti pamoja na msingi wa nadharia. Sura ya pili imetalii aina mbalimbali za unyanyasaji unaowakabili wanaume na misingi yake katika kazi zilizoteuliwa. Sura ya tatu imejadili athari za dhuluma dhidi ya wanaume. Sura ya nne imehakiki kazi za waandishi wa kiume na wa kike katika kuwalinganisha na kutofautisha mitazamo yao kuhusu swala la unyanyasaji dhidi ya wanaume. Sura ya tano ni hitimisho linalotoa muhtasari wa sura zote na matokeo ya utafiti huu. Pia mapendekezo ya tafiti za baadaye yametolewa.
Description
The PL 8704.U5 G5
Keywords
Swahili literature--Study and teaching
Citation