Tathmini ya hadithi za watoto katika mtandao
Loading...
Date
2015
Authors
Gatwiri, Joy Njue
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulinuia kutathrnini hadithi za watoto katika mtandao. Hadithi mbalimbali za
watoto zilichunguzwa arnbazo ni: visasili, hekaya, hurafa na hadithi zinazotokana na
methali. Njia rnbalimbali za matumizi ya mtandao ziliangaziwa arnbazo ni matumizi ya
mtandao kama kifaa cha kutolea matangazo na waandishi na wachapishaji ambao
huonyesha bei mbalimbali ya vitabu. Pia mtandao kama maktaba ambapo watoto
wanaweza kutumia muda wao kuzisoma hadithi katika mtandao. Pia nj ia tofauti ambazo
zimetumiwa kuwasilisha hadithi hizo ambazo ni kwa maandishi ambayo yanaweza
kusomwa na matumizi ya vielelezo. Utafiti pia uliangazia hadithi ambazo zimechapishwa
na zile arnbazo hazijachapishwa. Nadharia ya utegernezi wa vyombo vya habari ya Ball-
Rokeach na Defleaur (1976) ilitumika ambayo ilisaidia kuelewa jinsi hadithi za watoto
zinavyoingiliana na vyombo vya habari ili kutirniza malengo matatu ambayo ni
maelewano, burudani na ufunzaji. Nadharia ya fasihi ya watoto ya J ungmeen (1999) pia
itatumiwa ili kuelewa jinsi fasihi ya watoto inavyotangamana na maendeleo ya
teknolojia. Utafiti huu uliendelezwa katika maktaba na kutalii tovuti mbalimbali . Utafiti
huu ulikuwa wa kimaelezo na ufafanuzi. Mbinu ya jumla ilitumika katika kuchanganua
data.
Description
Tasnifu iliyowasilishwa katika idara ya kiswhili na lugha za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa minajili ya kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili, 2015