Mabadiliko ya Kihistoria katika Fonolojia ya Kiswahili: Udondoshaji wa Fonimu

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriamen_US
dc.contributor.advisorLeonard Chacha Mwitaen_US
dc.contributor.authorKiplimo, Cheruiyot Evans
dc.date.accessioned2022-04-01T08:44:15Z
dc.date.available2022-04-01T08:44:15Z
dc.date.issued2021
dc.descriptionTasnifu hii Imewasilishwa Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Desemba, 2021en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulichunguza mabadiliko ya kihistoria ya udondoshaji wa sauti za likwidi katika maneno ya Kiswahili. Kimsingi, silabi katika lugha huchukua mfumo wa konsonanti (K) kabla ya vokali (V) na huwakilishwa kama KV (Oostendorp, 2005 & Yule, 2010). Muundo wa silabi ya KV upo katika Kiswahili. Hyman (2003b) anabaini kuwa, silabi inayokubalika katika Mame-bantu imebanwa katika miundo ya KV, KVV na V. Miundo hii ya silabi ipo katika Kiswahili na baadhi yake ni matokeo ya mabadiliko ya kihistoria ya udondoshaji wa fonimu. Fonimu /l/ na /r/ zina mazoea ya kudondoshwa katika mazingira mahususi japo ithibati hazijatolewa. Utafiti huu ulichanganua maneno arubaini yaliyokusanywa kutoka Kamusi Kuu ya Kiswahili (2015). Malengo ya utafiti ni pamoja na kudhihirisha udondoshaji wa fonimu /l/ na /r/ katika maneno ya Kiswahili, kueleza sababu zake kutokea na kubainisha athari zake katika fonolojia arudhi ya Kiswahili. Nadharia ya fonolojia zalishi ya Chomsky na Halle (1968) iliteuliwa kuongoza utafiti huu. Mbinu ya uundaji ndani na mbinu linganishi zilitumiwa kupata ithibati iliyotumiwa kuthibitisha udondoshaji huu. Kwa kutumia mbinu ya uundaji ndani, maumbo awali ya maneno ya sasa yalionyeshwa na udondoshaji uliotokea na pale ambapo ushahidi ulikosekana, mbinu linganishi ilitumika kulinganisha maneno ya Kiswahili na mengine ya mnasaba (Ekegusii, Kikuyu, Kiluhya, Kimeru, Kitaita na Kikamba). Data ya maktabani iliwekea msingi upataji wa data ya nyanjani ambayo ilikusanywa kupitia kwa maswali ya hojaji. Sampuli ya maneno iliyofaa katika utafiti huu iliteuliwa kimaksudi pamoja na walengwa watano katika lugha zilizoteuliwa. Hatua hii ilikuwa muhimu kwa sababu mtafiti aliweza kulinganisha, kulinganua na kuunda upya leksika ya Kiswahili. Data ilichanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya kimaelezo, majedwali na unukuzi wa sheria za kifonolojia. Utafiti huu ulibaini kuwa fonimu za likwidi hudondoshwa katika mazingira ya kuwepo katikati ya vokali mbili. Kando na hayo, utafiti ulionyesha kuwa fonimu za likwidi zilidondoshwa kwa sababu ya haja ya kurahisisha matamshi na utashi wa wazungumzaji. Fonimu hizi zinapodondoshwa lugha hupata miundo changamano kifonetiki na hata kwenye miundo ya silabi. Udondoshaji unapotokea katika vitenzi teule, badiliko lingine (uchopekaji) linatokea ili kuhifadhi sheria ya uziada na kuleta mfumo unaokubalika. Utafiti huu uligundua kuwa, sheria ya udondoshaji wa kihistoria wa fonimu za likwidi haina tija katika Kiswahili cha sasa kwa sababu baadhi ya maneno yana mazingira ya udondoshaji ilhali udondoshaji hautokei. Utafiti huu unaweza kuendelezwa kwa kutumia nadharia nyinginezo pamoja na data ya asili tofauti kama vile kwenye hifadhi ya maandiko. Utafiti huu ulitoa mchango katika isimu historia na fonolojia ya Kiswahili.en_US
dc.description.sponsorshipChuo Kikuu cha Kenyattaen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/23468
dc.language.isootheren_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.subjectMabadilikoen_US
dc.subjectKihistoriaen_US
dc.subjectFonolojia ya Kiswahilien_US
dc.subjectUdondoshajien_US
dc.subjectFonimuen_US
dc.titleMabadiliko ya Kihistoria katika Fonolojia ya Kiswahili: Udondoshaji wa Fonimuen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Mabadiliko ya Kihistoria ....pdf
Size:
1.18 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Fultext thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: