Athari ya Tamthilia ya Mashetani (1971) juu ya Tamthilia ya Mashetani Wamerudi (2016)
Loading...
Date
2025-05
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuchunguza athari ya tamthilia ya Mashetani (1971) juu ya tamthilia ya Mashetani Wamerudi (2016). Kristeva (1966) anafafanua kuwa hakuna matini yoyote ya kifasihi inaweza kuangaliwa kivyake au kujitegemea. Hivyo basi, ilikuwepo haja kuangazia athari ya dhamira, maudhui, wahusika na mtindo katika tamthilia hizi teule. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Mwingilianomatini ilioasisiwa na Kristeva (1966). Mwingilianomatini ni kutegemeana na kuathiriana kwa tanzu au matini (Kuloba, 2015). Hivyo basi, mwingilianomatini ni wakati ambapo sifa za matini moja huweza kujitokeza katika matini nyingine. Mtafiti aliongozwa na malengo yafuatayo: Kwanza, kubainisha athari ya kimaudhui katika tamthilia ya Mashetani na tamthilia ya Mashetani Wamerudi. Pili, kuchunguza athari ya usawiri wa kiwahusika katika tamthilia ya Mashetani na Mashetani Wamerudi. Tatu, kuchanganua athari ya kimtindo katika tamthilia ya Mashetani na tamthilia ya Mashetani Wamerudi. Mbinu ya utafiti iliyotumika ni ya kimaelezo ambapo mtafiti alibainisha matukio au data mbalimbali katika tamthilia ya Mashetani na Mashetani Wamerudi. Data iliyokusanywa iliwasilishwa kwa maelezo na kwa kutoa mifano ya maudhui, usawiri wa wahusika na mtindo kwenye tamthilia zilizoteuliwa. Mtafiti aliteua sampuli kimakusudi ili kufanikisha malengo ya utafiti. Utafiti ulikuwa wa maktabani ambapo mtafiti alisoma tamthilia husika, tasnifu, majarida na vitabu ambavyo vinahusiana na mada.
Description
Tasnifu ya Utafiti Imetolewa ili Kutosheleza baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika, Mei 2025.
Msimamizi
Jesse Murithi