Ukiushi kama Mbinu ya Kudhihirisha Itikadi ya Kuumeni katika Fasihi ya Kiswahili Mifano kutoka Riwaya za Said Ahmed Mohamed na Euphrase Kezilahabi”, in Kiswahili na Utaifa Nchini Kenya
dc.contributor.author | Osore, Miriam | |
dc.contributor.author | Ryanga, Charlotte | |
dc.date.accessioned | 2023-11-22T16:53:30Z | |
dc.date.available | 2023-11-22T16:53:30Z | |
dc.date.issued | 2012 | |
dc.description | Book Chapter | en_US |
dc.description.abstract | Dhana ya ukiushi (defamiliarization) ina ma~na ya kudhihirisha kitu au hali kwa njia isiyokuwa ya kawaida, au isiyo dhahiri. Dhana hii hutumiwa kuele~a kijumla hali arnbapo kitu fulani hudhihirishwa kwa njia isiyo kuwa ya kawaida. Stacy (1977:178)anaeleza kwamba mbinu ya ukiushi inaweza kutumiwa kwa malengo mbalimbali; kama kuchekesha, kushangaza, kuhuzunisha, kukasirisha au kumfanyia mtu mzaha. 'Hata hivyo, mbinu hii imetumiwa kueleza uvumbuzi mpya arnbao umebadilisha maisha, na fikra za binadamu. Mbinu hii inapotumiwa katika fasihi huwa imetumiwa kimaksudi ili kudhihirisha jambo fulani. Mbinu ya ukiushi ina historia ndefu katika utunzi wa fasihi. Wananadharia na wanafasihi wamekiri, kwa mfano, kwamba mbinu ya ukiushi haiwezi kuepukika katika utunzi wa ushairi. Tangu awali, matumizi ya mbinu hii ya ukiushi yameelekea kusisitiza wazo kwamba, mbinu hii huturniwa kwa malengo mawili: kiujumi na kudhihirisha maana katika fasihi. George Steiner (1976:217~218),kwa mfano, anasema, "Lugha ndicho kifaa muhimu ambacho binadamu anaweza kutumia kukataa kuuona tilimwengu jinsi ulivyo". Anachosisitiza katika madai haya ni kwamba lugha hutumiwa kukiuka maana ya kawaida na kuvumbua njia mpya za kuuona ulimwengu. Dhana ya ukiushi katika fasihi iliasisiwa na mwanamaumbo mrusi Viktor Shklovsky ambaye aliunda dhana ya Kirusi 'Ostranenie' ambayo ilitafsiriwa ..katika Kiingereza kama "kueleza kwa njia ya ajabu" (making strange). Aliamini kwarnba jukumu la fasihi lilikuwa kueleza au kubainisha ulimwengu kwa njia isiyokuwa ya kawaida. Alikiri kwamba jukumu lafasihi KlSWAHILl NA UTAIFA NCHINI KENYA 121 I lilikuwa kuchochea hisia za msomaji. Kwake 'Ostranenie' ilijumlisha mbinu zote ambazo mwandishi wa fasihi anaweza kuturnia ili kubainisha kitu cha kawaida kwa njia ya kukifanya kieleweke kwa njia mpya. Kwa hivyo, alichukulia kwamba mbinu za ukiushi zililenga sio tu kudhihirisha maana, bali pia kutoa picha ya kipekee ya kile ambacho kilikuwa kikielezwa (Shklovsky 1965). Mbinu hizi zinapotumiwa katika fasihi, hutufanya kuona mambo kwa njia iliyo tofauti kabisa na jinsi tunavyoyajua. Mbinu za ukiushi ni muhimu kwa sababu msomaji wa fasihi huzitarnbua moja kwa moja anaposoma. Anapokutana na mbinu hizi, yeye hulazimishwa kuzifikiria na kisha kutambua ile maana mpya inayokusudiwa na mwandishi. Mbinu hizi ni nyingi na huweza kuwa za kitamathali kama vile jazanda, taswira, tashihisi, tashbihi na methali. Makala hii inafafanua jinsi Euphrase Kezilahabi na Said Ahmed Mohamed wanavyoshughulikia na kubainisha itikadi ya kuumeni (patriarchal ideology) kupitia mbinu za ukiushi. Watafiti wengi wameshughulikia mbinu mbalimbali za fasihi lakini si wengi ambao wamejaribu kuonyesha jinsi uhakiki wa mbinu za ukiushi unavyoweza kutumiwa kuelewa maana katika kazi za fasihi. Msimamo wetu ni kwamba mbinu za ukiushi ni muhimu katika utunzi wa fasihi na uchunguzi wa mbinu hizi unaweza kubainisha maudhui ya mwandishi kwa njia nzuri zaidi, | en_US |
dc.identifier.citation | Miriam Osore & Charlotte Ryanga (2012): “Ukiushi kama Mbinu ya Kudhihirisha Itikadi ya Kuumeni katika Fasihi ya Kiswahili Mifano kutoka Riwaya za Said Ahmed Mohamed na Euphrase Kezilahabi”, in Kiswahili na Utaifa Nchini Kenya (edited by Momanyi, C. et. al.), Nairobi, Twaweza Communications, Nairobi, pp 121 – 132. ISBN 978 9966 028 365. | en_US |
dc.identifier.issn | 978 9966 028 365 | |
dc.identifier.uri | http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/27184 | |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | Twaweza Communications | en_US |
dc.title | Ukiushi kama Mbinu ya Kudhihirisha Itikadi ya Kuumeni katika Fasihi ya Kiswahili Mifano kutoka Riwaya za Said Ahmed Mohamed na Euphrase Kezilahabi”, in Kiswahili na Utaifa Nchini Kenya | en_US |
dc.type | Book chapter | en_US |
Files
Original bundle
1 - 1 of 1
Loading...
- Name:
- Ukiushi Kamambinu Yakudhihirisha Itlkadi Yakuumeni Katlkafasihi ya Kiswahili Mifano Kutoka Riwayaza Said Ahmed Mohamed na Euphrasekezllahabi.pdf
- Size:
- 5.35 MB
- Format:
- Adobe Portable Document Format
- Description:
- Full text Book Chapter
License bundle
1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
- Name:
- license.txt
- Size:
- 1.71 KB
- Format:
- Item-specific license agreed upon to submission
- Description: