Itikadi na Ufundishaji wa Nadharia za Uhakiki wa fasihi

Loading...
Thumbnail Image
Date
2015
Authors
Wafula, R. M.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
UFUNDISHAJIwa nadharia za uhakiki wa fasihi ulipoanza, ilifikiriwa kwamba hatimaye fasihi imefanikiwa kupata silaha za kiuhakiki na kiakademia za kutegemewa. Wahakiki na wananadharia wa Kimagharibi kama Wellek na Warren (1946) walifikiria kwamba nadharia ya uhakiki wa fasihi ilikuwa moja popote fasihi iliposomwa. Hivi sasa katika kame ya 21, nadharia ni nyingi na zinaendelea kuundwa kuendana na mazingira anuwai ambamo wahakiki wanapatikana. Makala haya yananuia kuonyesha kwamba wingi wa nadharia zilizopo unaashiria mchomozo wa itikadi zinazoratibisha kuwepo kwa nadharia hizo . Japo Wellek na Warren walikuwa wakizungumzia kuhusu nadharia katika umoja wake, walikuwa wakiitikia maswala ya kiitikadi. Jambo hili linahusu fasihi ya Kiswahili vilevile.
Description
Conference Precentation
Keywords
Nadharia, Uhakiki, Itikadi
Citation