Mwathiriano Kati ya Watunzi wa Riwaya ya Kiswahili: Mwangwi wa Maudhui ya Mafuta (2008) katika Cheche za Moto (2008)

dc.contributor.authorKalingwa, Felix Musyoka
dc.contributor.authorKaui, Titus Musyoka
dc.date.accessioned2024-07-05T11:52:37Z
dc.date.available2024-07-05T11:52:37Z
dc.date.issued2023-10-18
dc.descriptionArticleen_US
dc.description.abstractMakala hii inashughulikia athari za Katama Mkangi kwa John Habwe kwa kujikita katika riwaya teule za Kiswahili za Mafuta (1984) na Cheche za Moto (2008). Utanzu wa riwaya ya Kiswahili umeendelea kupanuka kimaudhui na kifani kutokana na juhudi za watunzi mbalimbali kama vile Katama Mkangi na John Habwe. Japo tafiti za awali zimetafitia suala la mwingiliano matini, tafiti nyingi zimejikita katika kazi za mtunzi mmoja. Utafiti wa kina ulihitajika kuchunguza namna utunzi wa Mafuta (1984) ulivyoathiri John Habwe alipoitunga riwaya yake ya Cheche za Moto (2008). Katama Mkangi aliandika riwaya ya Mafuta katika wakati wa chama kimoja cha kisiasa ambapo uhuru wa kujieleza ulikuwa umebanwa sana. Habwe ameandika kazi yake katika mazingira yaleyale lakini katika kipindi ambapo uhuru wa kujieleza umepanuliwa. Kwa hivyo, amekwepa mtindo wa kimajazi alioutumia Mkangi na kuyaangazia masuala anayoyaibua kwa njia wazi. Makala hii ililenga kuonyesha kuwa maudhui katika riwaya ya Cheche za Moto ni mwangwi unaotokana na riwaya ya Mafuta (1984). Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya mwingiliano matini iliyoasisiwana Julia Kristeva (1969). Mihimili mikuu ya nadharia hii iliyoongoza utafiti huu ni pamoja na: hakuna matini ya fasihi yenye sifa za pekee, matini hubainisha sifa mbalimbali za matini tangulizi, na mwisho, matini ya baadaye huweza kufafanua dhana fulani kutoka matini tangulizi kwa njia inayoeleweka. Nadharia hii ya mwingiliano matini ilisaidia pakubwa kuonyesha namna kazi ya awali, Mafuta (1984) ilivyomwathiri John Habwe katika utunzi wa Cheche za Moto (2008) kimaudhui. Riwaya teule ziliteuliwa kimakusudiili kupata sampuli faafu yenye data ya kujaza pengo la utafiti. Data ilikusanywa kupitia kwa usomaji wa maktabani na vilevile kusakura mitandaoni kuhusu vipengele vya mwingiliano matini katika riwaya ya Kiswahili. Data hii imewasilishwa kwa njia ya kimaelezo. Utafiti wa makala hii unatarajiwa kutoa mchango katika uhakiki wa utanzu wa riwaya ya Kiswahili, hususan kuhusu kipengele cha kuathiriana baina ya watunzi wa riwaya za Kiswahilien_US
dc.identifier.citationKalingwa, F. M. & Kaui, T. M. (2023). Mwathiriano Kati ya Watunzi wa Riwaya ya Kiswahili: Mwangwi wa Maudhui ya Mafuta (2008) katika Cheche za Moto (2008).East African Journal of Swahili Studies, 6(1), 394-402. https://doi.org/10.37284/jammk.6.1.1524en_US
dc.identifier.urihttps://www.journals.eanso.org/index.php/eajss/article/view/1524/2186
dc.identifier.urihttps://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/28422
dc.language.isoenen_US
dc.publisherEAJSSen_US
dc.subjectAtharien_US
dc.subjectMwingilianoen_US
dc.subjectMatinien_US
dc.subjectWatunzien_US
dc.subjectRiwayaen_US
dc.titleMwathiriano Kati ya Watunzi wa Riwaya ya Kiswahili: Mwangwi wa Maudhui ya Mafuta (2008) katika Cheche za Moto (2008)en_US
dc.typeArticleen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Mwathiriano Kati ya Watunzi wa Riwaya ya Kiswahili....pdf
Size:
254.75 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Fulltext article
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: