Usawiri wa vijana katika tamthiilia teule za Kiswahili

dc.contributor.authorKaui, Titus Musyoka
dc.date.accessioned2011-11-07T12:38:34Z
dc.date.available2011-11-07T12:38:34Z
dc.date.issued2011-11-07
dc.descriptionThe PL 8704.K3U8en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulidhamiria kuchunguza usawiri wa vijana katika tamthilia teule za Kiswahili. Mtafiti amechanganua taswira mbali mbali zilizoibuka katika tamthilia hizi teule. Imebainika kuwa, taswira hizi ni kiwakilishi cha njia wanazotumia vijana kujipa mamlaka na kuyatumia, pamoja na mamlaka hayo kutumika kwao. Tasnifu hii imeonyesha kuwa, vijana wana uwezo wa kujipa mamlaka na kuyatumia sawa na wazee katika jamii. Hata hivyo, njia za kufanya hivyo ni tofauti na zile za wazee! Nadharia ya Ki-Foucault imetumika katika kuchanganua taswira zilizoibuka katika tamthilia teule. Nadharia hii huonyesha namna ambavyo mahusiano ya kijamii husawiri kinyang'anyiro cha matumizi ya mamlaka. Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia vipengele vya kimsingi katika tasnifu hii. Vipengele hivi vimeonyesha dhana muhimu kama zilivyotumiwa katika utafiti huu, namna suala la utafiti lilivyochipuka, malengo na misingi ya nadharia iliyoongoza utafiti huu, mapitio ya maandishi na mbinu za utafiti zilizotumika. Sura ya pili imejadili usawiri wa vijana katika asasi mbali mbali za kijamii. Katika sura hii dhana ya kijana, utamaduni wa vijana, mielekeo kuwahusu vijana, na hali zao duniani, zimefafanuliwa. Katika sura ya tatu, taswira za vijana katika tamthilia za Wakati Ukuta (1971) na Uasi (1980) zimechunguzwa. Tamthilia hizi zinawakilisha Ale za awali katika utunzi wa tamthilia ya Kiswahili. Sura ya nne imechanganua taswira za vijana katika tamthilia za Kitumbua Kimeingia Mchanga (2000) na Pango (2003). Tamthilia hizi ni kiwakilishi cha utunzi wa sasa katika historia ya tamthilia ya Kiswahili. Katika sura ya tano, muhtasari, matokeo ya utafiti, matatizo yaliyojiri katika utafiti na mapendekezo ya utafiti, yametolewa. Mwisho wa tasnifu hii ni marejeleo na kiambatisho.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/1601
dc.language.isoenen_US
dc.subjectSwahili literature--History and criticism//Youth in literature//Hussein,E.N. Wakati ukuta--History and criticism//Mohamed,S.A.Kitumbua kimeingia mchanga--History and criticism//wamitila, K.W.Pango--History and criticism//Kitsao, H.Uasi--History and criticismen_US
dc.titleUsawiri wa vijana katika tamthiilia teule za Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Usawiriwa vijana katika tamthilia teuleza.pdf
Size:
5.13 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
2.68 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: