Uchanganuzi wa methali za kiswahili: mtazamo wa kiudenguzi

dc.contributor.authorMurithi, Moses Murega
dc.date.accessioned2016-02-12T08:49:39Z
dc.date.available2016-02-12T08:49:39Z
dc.date.issued2015
dc.descriptionTasnifu hii imewasilishwa katika idara ya kiswahili ili kutosheleza sehemu ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, 2015en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umezichanganua methali za Kiswahili kwa mtazamo wa kiudenguzi. Utafiti huu umefanywa ikizingatiwa kuwa maana za matini hujiahirisha kwa ambavyo hakuna matini iliyo na maana moja. Sababu kuu ya kuchagua mada hii ilikuwa kubainisha kuwa baadhi ya methali za Kiswahili zina dhima hasi kwa jamii kinyume na dhana ya kijumla kuwa methali zote zina dhima chanya ambayo ndiyo tu imekuwa ikiangaziwa. Kwa misingi hii, malengo ya utafiti huu yamekuwa kutambua miktadha ya matumizi ya methali za Kiswahili zenye dhima hasi, kuziainisha methali za Kiswahili zenye dhima hasi kutegemea uhasi wake na kutambua manufaa ya methali za Kiswahili zenye dhima hasi kwa jamii. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya Udenguzi. Nadharia ya Udenguzi iliufaa utafiti huu kwa kuwa inawiana na lengo kuu la utafiti ambalo ni kuonyesha kuwa baadhi ya methali za Kiswahili zina maana hasi; maana hii inaweza kupatikana tu kwa kuzidengua. Data zilizotumika katika utafiti zilikusanywa maktabani ambapo kupitia usomaji methali za Kiswahili zinazopatikana katika kamusi mbalimbali za methali zilihakikiwa kwa makini na kubainisha dhima iliyomo; yaani uchanya au uhasi wake. Baada ya data (methali zenye dhima hasi) kukusanywa ziliainishwa kulingana na ujumbe uliomo kisha zilichanganuliwa kutegemea ujumbe husika na hususan kuzingatia dhima ya methali husika. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa methali zenye dhima hasi kama kuchochea vita, kudharau wanyonge, kuvunja moyo, kudhihaki ulemavu na zenye ubaguzi wa kikabila, kiuana na kiumri zipo. Matokeo ya utafiti yamewasilishwa kwa kuzingatia malengo ya utafiti na nadharia teule. Utafiti huu umegawika katika sura tano ambazo ni utangulizi uliochukua sura ya kwanza huku muktadha wa matumizi ya methali zenye dhima hasi ikichukua sura ya pili. Sura ya tatu inahusisha uchanganuzi wa methali za Kiswahili zenye dhima hasi kwa misingi ya nadharia ya Udenguzi. Aidha, sura ya nne imejikita katika uchunguzi wa manufaa ya methali zenye dhima hasi zilizochanganuliwa katika sura ya tatu kwa jamii huku sura ya tano ikibeba hitimisho na mapendekezo kwa utafiti zaidi.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/14157
dc.language.isoenen_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.titleUchanganuzi wa methali za kiswahili: mtazamo wa kiudenguzien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Uchanganuzi wa methali.....pdf
Size:
76.53 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text Thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: