Tathmini ya Usimulizi Katika Mahubiri ya Kiswahili kwa Watoto: Muktadha Wa Kanisa la Kiadventista Katika Kaunti ya Nakuru, Kenya

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorMasika, Rogers Mulwa
dc.date.accessioned2025-07-11T08:10:57Z
dc.date.available2025-07-11T08:10:57Z
dc.date.issued2023-06
dc.descriptionTasnifu hii Imetolewa ili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Juni 2023.
dc.description.abstractUtafiti huu ulinuia kuchunguza usimulizi katika mahubiri ya Kiswahili kwa watoto katika kanisa la Kiadventista. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza dhamira na maudhui ya masimulizi katika mahubiri kwa watoto, kuchunguza mbinu zilizotumika kuwasilisha masimulizi katika mahubiri kwa watoto na kuchunguza jinsi wahusika walivyosawiriwa katika masimulizi kwa watoto. Nadharia ya naratolojia iliyoasisiwa na Todorov mwaka wa 1969 pamoja na nadharia ya semiotiki iliyoasisiwa na Pierce (1977) ilitumika kuongoza utafiti huu. Kwa mujibu wa Todorov, nadharia ya naratolojia hubaini sifa za masimulizi na zinavyojitokeza katika miktadha mahsusi. Nadharia ya semiotiki inahusu ufasiri wa maana kutokana na ishara. Data zilikusanywa nyanjani kwa kutumia mbinu ya kuchunza au ushuhudiaji. Mtafiti alihudhuria ibada katika makanisa teule ya Kiadventista na kurekodi mahubiri hayo na kisha kuyasikiliza na kuyanakili kwa maandishi. Hatimaye, data zilichanganuliwa kwa kuongozwa na nadharia ya naratolojia na semiotiki. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha kuwa hadithi nyingi za watoto zilihusu maadili na kwa hivyo wasimulizi walikusudia kuwafundisha watoto kuzingatia maadili mema katika Jjamii. Aidha, matokeo ya utafiti huu yalionyesha kuwa matumizi ya masimulizi huboresha usikivu wa watoto. Kwa hivyo, utafiti huu una manufaa kwa walimu na wahubiri wa watoto hasa katika kuteua ujumbe ufaao na unaowajenga watoto kimaadili na pia kutumia mbinu ya uwasilishaji ambayo itawafanya watoto kuchangamkia ujumbe.
dc.identifier.urihttps://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/30351
dc.language.isoother
dc.publisherKenyatta University
dc.titleTathmini ya Usimulizi Katika Mahubiri ya Kiswahili kwa Watoto: Muktadha Wa Kanisa la Kiadventista Katika Kaunti ya Nakuru, Kenya
dc.typeThesis
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Tathmini ya usimulizi katika.......pdf
Size:
2 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
2.66 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: