Mnyambuliko wa vitenzi vya Lulogooli: mtazamo wa fonolojia leksia

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011-11-08
Authors
Mayodi, David Adenya
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu ulinuia kushughulikia mnyambuliko wa vitenzi vya Lulogooli. Lengo kuu lilikuwa kubainisha namna nadharia ya fonolojia leksia ifvyo toshelevu na mwafaka katika kushughulikia mnyambuliko huo. Utafiti ulifanywa kwenye taarafa ya Vihiga, Wilaya ya Vihiga katika Mkoa wa Magharibi, nchini Kenya. Jumla ya kata nne zilishirikishwa kwenye kazi hii nazo ni: Wamuluma, Mungoma, Maragoli ya kati na Maragoli kusini. Kata hizi zilishirikishwa kwa sababu inaaminika huko ndiko kuliko kitovu chao na kwamba lugha inayozungumzwa huko haijaathiriwa pakubwa na majirani zao. Utafiti ulikuwa na malengo manne ambayo ni kutambua na kubainisha taratibu za mnyambuliko wa vitenzi vya Lulogooli, kudhihirisha mifanyiko ya sauti inayoandamana na mnyambuliko huo, kubainisha kanuni na vigezo vinavyofuatwa kwenye mnyambuliko wake na kisha kutathmini maana mbalimbali zilizosetiriwa katika mnyambuliko huo. Utafiti umehusisha mbinu mbili kuu za utafiti yaani wa maktabani na nyanjani. Ili kufanikisha malengo yake, mazungumzo ya wasemaji wazawa wa lugha hii yalinaswa katika eneo la utafiti katika miktadha mbalimbali ili kupata vitenzi vinavyoeleza dhana na hali mbalimbali. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kwamba vitenzi vya Lulogooli vinanyambuliwa kwa namna maalum kwa kuzingatia sheria bayana za kifonolojia na unahusisha mabadiliko mbalimbali ya kifonolojia. Kazi hii imedhihirisha kuwa nadharia ya fonolojia leksia ni mwafaka katika kushughulikia mnyambuliko huo kwa kuzingatia mihimili yake ya nadharia hiyo.
Description
The PL 8474 .L8M3
Keywords
Lulogooli language -- Kenya//Lulogooli language -- Verb//Grammar, Comperative and general -- Verb//Lulogooli language -- Phonology
Citation