Uhuru wa kishairi katika utunzi wa mashairi: uchanganuzi wa sikate tamaa na miale ya uzalendo
Loading...
Date
2016-05
Authors
Munyao, Meshack Kimeu
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulishughulikia matumizi ya uhuru wa kishairi katika utunzi
wa mashairi: uchanganuzi wa Miale ya Uzalendo na Sikate tamaa.
Utafiti huu ulifanywa kwa lengo la kuwasaidia wasomaji wakiwemo
walirnu na wanafunzi kuuelewa ushairi wa Kiswahili. Utafiti huu
'uliongozwa na malengo haya: kubainisha mbinu mbalimbali za uhuru
wa kishairi, kuonyesha namna uhuru wa kishairi unavyobainika katika
kazi hizi mbili na kueleza sababu za msanii kutumia uhuru wa kishairi.
Ili kuyafikia malengo haya utafiti huu uliongozwa na nadharia ya
upokezi. Nadharia hii inamwangazia msomaji na tajriba yake ya kazi
ya fasihi tofauti na nadharia za zamani zilizolenga mwandishi na
matini yen yewe. Nadharia hii inamtambua msomaji kama kiungo
muhimu ambacho kinaipa kazi ya fasihi kuweko na hivyo kukaniilisha
maana yake kupitiaufasiri rnwema-Utafiti huu ulifanyiwa maktabani.
Pia huduma za rntandao zilitumiwa hasa kupata wasifu wa waandishi
wa diwani hizi na maelezo zaidi ya nadharia. Vitabu vilivyochunguzwa
ni Miale ya Uzalendo na Sikate Tamaa. Tasnifu hii ina sura tano.
Sura ya kwanza ina sehemu zifuatazo; utangulizi wa tasnifu, mada ya
utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na
mipaka ya utafiti, udurusu wa mada, misingi ya nadharia na mbinu za
utafiti. Sura ya 'pili imeshughulikia sifa za ushairi wa Kiswahili hasa
lugha na ushairi wa Kiswahili. Aidha imeangazia wasifu wa wasanii;
Mohamed S.A na Kitula King'ei. Mwishowe ikaangazia mbinu
mbalimbali za uhuru wa kishairi zinazotumika katika utunzi wa
mashairi. Katika sura ya tatu, tasnifu imeangazia matokeo ya utafiti;
yaani jinsi uhuru wa kishairi ulivyo tumika katika diwani; Miale ya
Uzalendo ya King'ei (1999). Sura ya nne imeonyesha namna uhuru wa
kishairi ulivyotumika katika Sikate Tamaa ya Mohamed (1980). Sura
ya tano imetoa muhtasari, hitimisho na mapendekezo ya utafiti. Utafiti
huu ni miongoni mwa tafiti chache ambazo zimefanywa kuhusuuhuru
wa kishairi. Utafiti utawafaidisha wasomi wengi wakiwemo
wahadhiri, walimu 'na wanafunzi wanaotafuta uelewa wa ushairi wa
Kiswahili. Aidha utawafaa wahakiki wengi wa fasihi ya Kiswahili
hususan mashairi.
Description
Tasnifu hii lmetolewa kwa idara ya kiswahill na lugha za katika Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa minajili ya kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika kiswahili.
May 2016, The PL 8704 .M82