Tathmini ya Kiwango cha Ubadilishaji Msimbo katika Vituo vya Moduli ya Masafa ya Mulembe na Moduli ya Masafa ya Sulwe
Loading...
Date
2023
Authors
Mabonga, Ivy
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulijikita katika kutathmini kiwango cha ubadilishaji msimbo katika vituo
viwili vya Royal Media Services ambavyo ni vya moduli ya masafa ya Mulembe na
Sulwe. Katika kituo cha Sulwe, lahaja ya Lubukusu imechukuwa nafasi ya lugha msingi
huku lahaja za Kiluhya haswa Lukabrasi, Luwanga, Lukhayo na lahaja zingine
zikichukuwa nafasi ya lugha msingi katika kituo cha Mulembe. Ijapokuwa lugha hizo
zinatumiwa katika mahojiano, matangazo na mambo mengine ya utangazaji wakati
mwingine wageni na watangazaji hutumia Kiswahili. Kwa hivyo, utafiti huu uliangazia
matumizi ya Kiswahili katika vituo hivyo ili kuweza kutathmini kiwango chake katika
ubadilishaji msimbo kupitia tathmini ya vichocheo vya ubadilishaji msimbo, ubainishaji
wa jinsi ubadilishaji msimbo hutokea na uchanganuzi wa athari zinazotokana na
ubadilishaji msimbo zinazojidhihirisha katika jamii hiyo. Kupitia malengo hayo, kiwango
cha ubadilishaji msimbo kiliweza kutathminiwa kwa kuchunguza matumizi ya Kiswahili
ambayo yalituwezesha kupima kiwango cha matumizi yake vituoni humo.Nadharia ya
Maki iliyoasisiswa na Myers –Scotton (1993) ndio iliyoongoza utafiti huu. Nadharia hii
ilijikita katika dhana za kutia na kutoa maki zilizowasilisha upya au ukawaida. Mkabala
huu ulilinganisha lugha kadhaa ili kuangazia sababu zinazopelekea lugha moja
kuchaguliwa kwa minajili ya matumizi miongoni mwa nyingine. Dhana ya kutia na kutoa
maki hutumika katika nadharia hii kujenga msingi wa kubainisha vichocheo vya
kisaikolojia na vya kijamii katika kuchanganuzi wa msimbo. Mbali na hayo, nadharia hii
inaelezea maswala mengine kama vile ustadi au uwezo wa kuwasiliana, ambayo
huchanganua maswala ya muktadha na ustadi.Mengine ni haki na majukumu ambayo
hudhihirisha mazingira ya kutoa au kutia maki katika msimbo. Utafiti huu ulifanyika
maktabani mno kwa kusoma tafiti na vitabu vilivyoandikwa kuhusu mada ambavyo
vilikuwa nguzo ya utafiti huu. Utafiti wa nyanjani ulifanyika katika vituo teule kupitia
usikilizaji wa baadhi ya vipindi na mahojiano na wanahabari wa vituo hivyo. Data
iliwasilishwa kwa njia ya kijarabati na kimaelezo, ili kuelezea na kuchanganua kikamilifu
semi zenye ubadilishaji msimbo. Utafiti huu utawafaidi watafiti tathmini ya matumizi ya
lugha katika jamii yenye wingi lugha iliyowekewa mipaka au huru. Kupitia ubainishaji
wa athari ya Kiswahili kwa Kiluhya na vichocheo vilivyobainishwa, wanaisimu jamii
wataweza kupima na kuchanganua mtagusano wa lugha kiidadi na kimaelezo.
Description
Evaluation of the Level of Code-Switching in Mulembe Frequency Modulation and Sulwe Frequency Modulation Tasnifu hii Imetolewa ili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili Katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Mei 2023.
Keywords
Ubadilishaji Msimbo, Moduli ya Masafa ya Mulembe, Moduli ya Masafa ya Sulwe