Nomino Ambatani za Kiswahili Zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano.

dc.contributor.authorAyiega, Mofart Onyoni
dc.contributor.authorMwita, Leonard Chacha
dc.date.accessioned2023-11-20T11:42:25Z
dc.date.available2023-11-20T11:42:25Z
dc.date.issued2021-10
dc.descriptionArticleen_US
dc.description.abstractMakala hii inachanganua nomino ambatani za Kiswahili zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano. Kanuni hii huonesha utaratibu wa kujenga neno kamili kwa kutumia vijenzi. Mabano katika kanuni hii hudhihirisha mipaka na hufutwa kuashiria kuwa sheria za uundaji wa maneno hazina ufikiaji wa muundo wa maneno yaliyotokana na ngazi za awali. Utafiti huu ulifanywa baada ya kubaini kuwa baadhi ya nomino ambatani za Kiswahili hukiuka Kanuni ya Kufuta Mabano hasa pale ambapo mabadiliko hutokea katikati mwa neno baada ya vipashio mbalimbali kuunganishwa. Nomino ambatani ifuatayo inadhihirisha mabadiliko yanayotokea katikati mwa neno baada ya vipashio mbalimbali kuunganishwa; [mw [enyekiti]] → [we [enyeviti]]. Katika utafiti huu tulikusanya data kutoka kwenye Kamusi Kuu ya Kiswahili (2015) ambapo nomino ambatani thelathini zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano zilitumika kama data ya msingi. Nomino hizi zilichaguliwa kwa kuzingatia sifa bainifu za ukiukaji wa Kanuni ya Kufuta Mabano (KKM). Utafiti huu uliongozwa na mhimili mmoja wa nadharia ya Mofolojia Leksia iliyoasisiwa na Kiparsky (1982) na kuendelezwa na Katamba na Stonham (2019): Kanuni ya Kufuta Mabano. Nadharia ya Mofolojia Leksia iliibuka kufidia mtazamo wa Chomsky wa Sarufi Zalishi ambao haukutambua kiwango cha mofolojia kama kiwango mahususi cha lugha. Kimsingi nadharia hii inaonesha uhusiano wa sheria zinazojenga maumbo ya kimofolojia na sheria zinazodhibiti namna maumbo hayo yanavyotamkwa. Data iliyohusiana na mada ya utafiti ilikusanywa maktabani. Baadhi ya makala ambazo zilitumika katika utafiti huu ni tasnifu za awali, makala ya mtandaoni na majarida. Utafiti huu uliongozwa na usampulishaji kimakusudi ili kufikia maneno husika ya nomino ambatani yaliyo na sifa bainifu. Matokeo ya utafiti huu yaliwasilishwa kwa njia ya michoro, majedwali na maelezo. Utafiti huu unachangia isimu hasa kupitia kuelewa na kueleza mbinu za mwambatano katika lugha ya Kiswahili, kuwahami waundakamusi za Kiswahili na maarifa, na kukuza mofolojia ya Kiswahili.en_US
dc.identifier.citationAyiega, M. O., & Mwita, L. C. (2021). Nomino Ambatani za Kiswahili Zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano. Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 4(1), 30-42.en_US
dc.identifier.urihttps://doi.org/10.37284/jammk.4.1.452
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/27148
dc.language.isoenen_US
dc.publisherEANSOen_US
dc.subjectMofimuen_US
dc.subjectMwambatanoen_US
dc.subjectUkiukajien_US
dc.subjectKanuni ya Kufuta Mabanoen_US
dc.subjectMabadilikoen_US
dc.subjectUtaratibuen_US
dc.titleNomino Ambatani za Kiswahili Zinazokiuka Kanuni ya Kufuta Mabano.en_US
dc.typeArticleen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Nomino Ambatani za Kiswahili Zinazokiuka....pdf
Size:
371.91 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text Article
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: