Maudhui na mtindo katika ushairi wa watoto: uchanganuzi wa utenzi wa haki za watoto na mashairi Bulbul
Loading...
Date
2018
Authors
Ngugi, Esther
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Mtindo na maudhui ni masuala mawili ambayo huchangizana na kukamilishana ili kufaulisha kazi ya sanaa. Utafiti ulichanganua maudhui na mtindo katika diwani teule za mashairi ya watoto. Nazo ni; Utenzi wa haki za Watoto (2003) cha Yusuf Abbas na Mashairi Bulbul (2010) cha Ahmed Hussein Ahmed. Malengo ya utafiti ni: Kubainisha maudhui yanayojitokeza katika mashairi ya watoto, kuchunguza mbinu za kimtindo zilizotumiwa na watunzi katika kufanikisha uwasilishaji na upokezi katika ushairi wa watoto katika diwani teule na kuonyesha umuhimu wa maudhui yaliyosawiriwa katika ushairi wa watoto. Nadharia mbili za uhakiki ziliongoza utafiti huu; nazo ni naharia ya kiuhalisia na nadharia ya kimtindo. Kimsingi, nadharia ya uhalisia iliyoasisiwa na Hegel imehutumiwa kuchanganua kazi ya kifasihi kwa kuangalia maudhui katika kazi husika kwa kuonyesha jinsi masuala yanayoangaziwa humo yanajitokeza katika jamii halisi. Nayo nadharia ya kimtindo iliyoasisiwa na Coombes hutumiwa kuchunguza mtindo katika misingi ya matumizi ya lugha katika kazi husika. Utafiti umekusanya data kutoka maandishi ya kazi hizi mbili, ambapo data ya kimsingi itapatikana kutokana na diwani teule. Katika kuendeleza kazi hii, uteuzi sampuli makusudi umetumiwa kuteua beti zilizochanganuliwa maudhui na mtindo. Data imechanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya kimaelezo kuambatana na malengo ya utafiti. Uwasilishaji wenyewe umefanywa kwa sura tano.
Description
Tasnifu iliyotolewa kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahadha ya uzamili katika Chuo Kikuu Cha Kenyatta. 2018