Athari za Ulevi katika Mshikamano wa Kijamii: Uchanganuzi wa Wahusika Teule katika Riwaya ya Dunia Mti Mkavu (S. A. Mohamed) na Rosa Mistika (E. Kezilahabi)

dc.contributor.authorMutugu, Beth N.
dc.contributor.authorOsore, Miriam Kenyani
dc.date.accessioned2023-11-22T15:07:24Z
dc.date.available2023-11-22T15:07:24Z
dc.date.issued2019
dc.descriptionBook Chapteren_US
dc.description.abstractKwa mujibu wa Swegan (2011), pombe ni mojawapo ya vinywaji ambavyo vinatumiwa katika tamaduni nyingi. Kinywaji hiki hutumiwa na watu wengi kama njia ya kujistarehesha, lakini ikiwa kitatumiwa kwa muda mrefu bila tahadhari, kinamfanya mtu kupata uraibu hasa iwapo hawezi kukaa kwa muda mrefu bila kukitumia. Kwa mujibu wa Kimble na wengine (1980), tabia ya unywaji pombe kupindukia huwaathiri watu wa kila tabaka: walioelimika, werevu, wasioelimika, matajiri, na maskini. Robin (1983) anasema kuwa pombe ni kinywaji ambacho kimekuwa kikimburudisha na kumtatiza binadamu kwa kame nyingi. Hata hivyo, unywaji wa pombe kupindukia ni maradhi yaliyofichika na hayatambuliki kwa urahisi. Kulingana na Torr (2000), kwa miongo kadha iliyopita kumekuwa na mwamko mpya ambapo uraibu wa pombe umetambulika kama swala la tiba badala ya suala la kimaadili arnbapo wataalamu wa tiba wamefumbua kuwa uraibu huu unaweza kukabiliwa kwa kutumia njia za kimatibabu. Katika mwaka wa 1951, Shirika laAfya Ulimwenguni (WHO) lilitambua uraibu wa pombe kama mojawapo ya magonjwa yanayoathiri wanajamii. Kwa mujibu wa Buckham (1971), matumizi ya pombe kama zilivyo dawa zingine za kulevya hurnfanya mtu kuwa na mazoea kiasi kwamba hawezi kujizuia kuitumia. Hali hii huathiri afya yake, utekelezaji wa majukumu na uhusiano wake na wanajamii wenzake. Robin (1983), anasema kuwa uraibu wa pombe ni ugonjwa. Kadhalika, matumizi mabaya ya pombe yanaweza kuhusishwa na visa vya mauaji, ugomvi wa nyumbani, kuzorota kwa afya na kutokea kwa ajali za aina mbalirnbali.K wa kuzingatia maoni ya wataalamu hawa, inabainika kuwa pombe huchangia katika kuzorotesha mshikamano na I' utangamano miongoni mwa wanajamii. Katika sehemu inayofuata athari za ulevi katika mshikamano wajamii zitachanganuliwa kwa kurejelea wahusika mahsusi katika riwaya ya Dunia Mti Mkavu (S.A. Mohamed) na Rosa Mistika (E. Kezilahabi).en_US
dc.identifier.citationMutugu, B. & Osore, M. (2019). Athari za Ulevi katika Mshikamano wa Kijamii: Uchanganuzi wa Wahusika Teule katika Riwaya ya Dunia Mti Mkavu (S. A. Mohamed) na Rosa Mistika (E. Kezilahabi), katika Lugha na Fasihi katika Mshikamano wa Kitaifa na Uwiano. (Wah) Kobia, Kandagor na Mwita (2019) uk. 239-250. Eldoret: Moi University Pressen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/27168
dc.language.isootheren_US
dc.publisherMoi University Press.en_US
dc.titleAthari za Ulevi katika Mshikamano wa Kijamii: Uchanganuzi wa Wahusika Teule katika Riwaya ya Dunia Mti Mkavu (S. A. Mohamed) na Rosa Mistika (E. Kezilahabi)en_US
dc.typeOtheren_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
Athari za Ulevi katika Mshikamano wa Kijamii Uchanganuzi wa Wahusika Teule katika Riwaya ya Dunia Mti Mkavu (S. A. Mohamed) na Rosa Mistika (E. Kezilahabi).pdf
Size:
6.48 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text Book Chapter
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: