Ushairi Unaotumia Methali Kama Mlezi wa Utamaduni katika Jamii
dc.contributor.author | Maitaria, J. N. | |
dc.date.accessioned | 2014-01-11T09:12:35Z | |
dc.date.available | 2014-01-11T09:12:35Z | |
dc.date.issued | 2012 | |
dc.description.abstract | Makala hii inahakiki mabadiliko ya kimtindo katika utunzi na uwasilishaji wa ushairi wa Kiswahili. Kwa mfano, hapo awali utungo huu ulitungwa kwa kuzingatia utamaduni wa Waswahili kama jamii. Kwa wakati wa sasa unatungwa na wasanii kutoka jamii pana ya Afrika Mashariki. Kipengele cha methali ni miongoni mwa zile maarufu katika tungo zilizozingatia mno arudhi za kimapokeo. Aidha, baadhi ya wasanii wanawasilisha tungo zao kwa kuzingatia zaidi kauli mahususi wanazobuni wanatumia kwa kadri au zile teule zinazopatikana katika mapokeo ya jamii. Katika muktadha huu, ushairi wa Kiswahili una sifa anuwai ambazo huweza kutumiwa kuubainisha. Kwa kuzingatia au kutozingatia matumizi ya methali katika uwasilishaji, tungo hizi zinaweza kuainishwa kimakundi. Kwa hivyo, ushairi wa kisasa wa Kiswahili unaweza kuwa ni ule unaozingatia methali zaidi, chache au ule unaoasi kabisa matumizi hayo. Swali ni kwamba, kati ya tungo zinazotumia au zile zisizotumia methali katika uwasilishaji wake ni zipi zilizo bora? | en_US |
dc.identifier.citation | Journal of Swahili Studies Vol. 1. | en_US |
dc.identifier.uri | http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/8504 | |
dc.language.iso | en | en_US |
dc.title | Ushairi Unaotumia Methali Kama Mlezi wa Utamaduni katika Jamii | en_US |
dc.type | Article | en_US |