Majazi na Stiari katika Riwaya ya Dunia Yao na Nyuso za Mwanamke

Loading...
Thumbnail Image
Date
2024-12
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulichunguza matumizi ya majazi na stiari katika riwaya mbili teule za Said Ahmed Mohamed nazo ni Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010). Utafiti huu ulilenga kubaini majazi na stiari katika kazi teule, nafasi ya majazi na stiari katika kuwasawiri wahusika na kuonyesha jinsi mtunzi ametumia tamathali hizi kuibua maudhui. Utafiti huu ulikuwa wa kimaelezo na wa maktabani. Uteuzi wa sampuli ulikuwa wa kimakusudi ukilenga riwaya za Said Ahmed Mohamed nazo ni Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010). Ukusanyaji wa data ulihusisha usomaji wa kina wa riwaya teule ili kupata data inayokusudiwa. Hizi ni riwaya ambazo zimesheheni matumizi ya majazi na stiari. Data ilichanganuliwa kwa kuongozwa na malengo ya utafiti pamoja na mihimili ya nadharia ya Mtindo na ile ya Matumizi ya Stiari. Nadharia ya Mtindo inashikilia kuwa kazi za kifasihi haziwezi kuibuliwa bila matumizi ya lugha nayo nadharia ya Matumizi ya Stiari hushikilia kuwa ili kuelewa dhana moja ya kistiari yafaa tuilinganishe na nyingine iliyo na sifa zile zile zinazorejelewa. Uwasilishaji wa data hiyo ulikuwa wa kimaelezo. Riwaya ya Dunia Yao (2006) na ile ya Nyuso za Mwanamke (2010) tulizozitafitia ziliandikwa mwanzo mwanzo wa Karne ya 21 na zilidhihirisha mkondo mpya wa kutunga kazi za kifasihi (ule wa usasa baadaye). Riwaya hizi zilisheheni matumizi mapya na ya kipekee ya majazi na stiari ambapo uwasilishaji wa uhalisia na usawiri wa wahusika sasa haufanywi kwa kufuata mkondo wa hurafa kama hapo awali bali unahusisha matumizi mapya ya majazi na stiari ambapo hadithi, wahusika, matukio na mandhari huweza kufasiriwa au kusomwa ili ziweze kuleta zaidi ya kiwango kimoja cha maana. Utafiti huu utawafaa wahakiki wa riwaya ya Kiswahili, wasomi na watunzi wa kazi za kifasihi kuona namna waandishi wa tungo za kifasihi wa Karne hii ya 21 wanavyotumia tamathali za usemi kwa njia ya kipekee kuwasilisha uhalisia.
Description
Tasnifu hii Imetolewa ili Kutosheleza baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Disemba 2024. Msimamizi Richard Wafula
Keywords
Citation