Swala la mwanamke katika tamthilia ya Kiswahili: waandishi katika njia-panda

dc.contributor.advisorChacha Nyaigotti-Chacha
dc.contributor.advisorCatherine Mwihaki Ndungo
dc.contributor.authorMule, Katwina
dc.date.accessioned2012-05-17T12:19:00Z
dc.date.available2012-05-17T12:19:00Z
dc.date.issued2012-05-17
dc.descriptionThe PL 8704.M8en_US
dc.description.abstractTasnifu hii ni uhakiki wa swala la mwanamke kama linavyojitokeza katika tamthilia za Kiswahili zilizoandikwa na waandishi wa kike. Tunachunguza taswira zinazojitokeza katika kila mojawapo ya kazi tulizozishughulikia. Kutokana na taswira hizi, tunauchambua msimamo wa mwandishi kuhusu swala la ukombozi wa wanawake. Uchunguzi huu umeibuka kutokana na imani kwamba wanawake ni kundi linalodhulumiwa katika jamii ya sasa kwa msingi ya uana wao. Tunaamini kwamba lazima swala la ukombozi wao lianze nao. Uchunguzi wetu basi unajaribu kunchunguza iwapo waandishi hawa ni watetezi halisi wa maslahi ya wanawake. Sura ya kwanza ni utangulizi. Hapa, tunazingatia somo la utafiti, madhumuni yake na upeo wa utafiti huu. Pia tumezungumzia kwa ufupi yale yalioandikwa kuhusu mada hii na kuelezea kwa muhtasari nadharia tunayoitumia kuzitathmini kazi tulizochagua. Hatimaye tunatoa sababu zilizotufanya kulichagua somo hili na kuonyesha njia tulizotumia kuufanya utafiti huu. Sura ya pili inawachambua waandishi wawili wa kipekee wa Kenya. Hawa ni Sheila Ali Ryanga na Ari Katini Mwachofi. Tumeonyesha kuwa waandishi hawa wanatofautiana kumaudhui, uendelezaji wa wahusika na kimtazamo. Hata hivyo, kwa njia moja au nyingine, wanaonekana kutokuwa na msimamo thabiti kuhusu swala la mwanamke. Sura ya tatu inazichunguza tamthilia mbili za Penina Muhando alizoziandika kati ya 1972 na 1974 na tamthilia moja ya Angelina Chogo aliyoiandika 1976. Hawa ni waandishi wa Tanzania. Tumeonyesha athari za siasa ya ujamaa kwa uchotaji na unendelezaji wa maudhui, wahusika na masuluhisho wanayoyapendekeza kwa matatizo yanayoikumba jamii yao; swala la mwanamke likiwemo. Sura ya nne ni Uchambuzi wa tamthilia mbili za Penina Muhando alizoziandika katika miaka ya themanini. Tumeonyesha jinsi mwandishi huyu anavyobadilika na kupevuka kimtazamo katika kazi hizi zikilinganishwa na zile nyingine za mwanzo. Sura ya tano ndiyo hitimisho ya kazi hii. Hapa, tunatoa muhtasari wa kazi yetu kwa jumla na kujadili kwa ufupi mambo muhimu yanayojitokeza katika kazi hizi. Pia tumetoa mapendekezo yetu kuhusu utafiti zaidi ambao ungefanywa kuwahusu waandishi hawa.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/4648
dc.language.isoenen_US
dc.subjectKiswahili drama womenen_US
dc.titleSwala la mwanamke katika tamthilia ya Kiswahili: waandishi katika njia-pandaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Swala la mwanamke katika tamthilia ya kiswahili.pdf
Size:
86.47 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full Text Thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
2.68 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: