Matumizi ya masimulizi na malumbano katika tamthilia ya kiswahili

dc.contributor.authorWakesho, Mwambi Phoebe
dc.date.accessioned2011-08-12T12:13:50Z
dc.date.available2011-08-12T12:13:50Z
dc.date.issued2011-08-12
dc.descriptionAbstracten_US
dc.descriptionDepartment of Education,217p.The PL 8704 .M85M3 2010
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia matumizi na malumbano katika tamthilia ya Kiswahili. Tamthilia zilizoshughulikiwa ni Wingu jeusi(1987) na pango(2003). Utafiti huu uliongozwa na nadharia mseto za uhakiki wa mwingilianomatini. Nadharia hizi zilifaa katika utafiti huu, hasa ikizingatiwa kwamba tmthilia hizi zilizotafitiwa zimesheheni matumizi ya masimulizi na malumbano. Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa mtafiti ameshughulikia mada ya utafiti,sababu ya kuchagua mada na yaliyoandikwa kuhusu mada hii. Pia amejadili upeo na mipaka ya utafiti huu na misingi ya nadharia zilizoongoza utafiti huu. Mwisho, mbinu za utafiti zimeelezwa. Sura ya pili imejadili asili ya fasihi, fasihi andishi sifa za tamthilia na mikondo yake, tofauti simulizi na andishi na maathiriano ya fasihi andishi na simulizi. imebainika kwamba waandishi wengine huathiriwa kifani, kimaudhi na kidhamira. Katika sura hii imebainika kwamba fasihi andishi haijavumbua dhamira mpya. Pia imebainika kwamba michezo mingi ya redio ambayo hupendwa sana na wasikilizaji ni fasihi simulizi. Utafika ulidhamiria kuhakiki jinsi fasihi simulizi inavyoiathiri tamthilia ya kiswahili katika kutumia masimulizi na malumbano kama mtindo wa uandishi. Sura ya tatu imechunguza jinsi wa masimulizi ulivyotumiwa katika tamthilia ya kiswahili. Pia sura hii imejadili historia fupi za waandishi wa tamthilia za wingu jeusi na pango ambao ni chacha na wamitila. Vile vile mihtasiri ya tamthilia za wingu jeusi na pango imeonyeshwa ili kumpa mtafiti mwelekeo kuhusu falsafa ya waandishi hawa. Sura ya nne imechunguza matumizi ya mtindo wa malumbano katika tamthilia za wingu jeusi na pango. Utafiti umebainisha kwamba malumbano huweza kusababishwa na maswala ya kijamii, kisiasa,kiuchumi,kidini na kadhalika. Pia imebainika kwamba malumbano huweza kuwa na athari hasi kama vile kukasirika,kutukanana,kudharauliana na kadhalika. Sura ya tano imejadili muhtasari wa utafiti huu. Pia imeonyesha matokeo ya utafiti, matatizo ya utafiti, mchango wa utafiti huu na mapendekezo ya mtafiti. Mwishowe kuna marejeleo ya utafiti huu. Utafiti huu pia ni miongoni mwa kazi chache ambazo zimewahi kuhakiki tamthilia za wingu jeusi na pango kwa kuzihusisha na vipera vya fasihi simulizi na pia kuzihakiki kwa kuzingatia nadhria mseto za uhakiki wa kimtindo na mwingilianomatini. Utafiti huu utawasaidia wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vikuu,n pia wanafunzi wa shule za upili,kwani somo la kiswahili linahusisha fasihi simulizi na andishi. Pia mtafiti anaamini kwamba utafiti huu utawafaidia wapenzi wote wa lugha ya kiswahili.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/755
dc.language.isoenen_US
dc.subjecthacha, Chacha Nyaigoti's Wingu jeusi --History and criticism
dc.subjectWamitila, Kyalo Wadi's Pango --History and criticism
dc.subjectSwahili drama --Kenya
dc.titleMatumizi ya masimulizi na malumbano katika tamthilia ya kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Mwambi Phoebe.pdf
Size:
6.9 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: