Matumizi ya masimulizi na malumbano katika tamthilia ya kiswahili

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011-08-12
Authors
Wakesho, Mwambi Phoebe
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia matumizi na malumbano katika tamthilia ya Kiswahili. Tamthilia zilizoshughulikiwa ni Wingu jeusi(1987) na pango(2003). Utafiti huu uliongozwa na nadharia mseto za uhakiki wa mwingilianomatini. Nadharia hizi zilifaa katika utafiti huu, hasa ikizingatiwa kwamba tmthilia hizi zilizotafitiwa zimesheheni matumizi ya masimulizi na malumbano. Tasnifu hii ina sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti. Hapa mtafiti ameshughulikia mada ya utafiti,sababu ya kuchagua mada na yaliyoandikwa kuhusu mada hii. Pia amejadili upeo na mipaka ya utafiti huu na misingi ya nadharia zilizoongoza utafiti huu. Mwisho, mbinu za utafiti zimeelezwa. Sura ya pili imejadili asili ya fasihi, fasihi andishi sifa za tamthilia na mikondo yake, tofauti simulizi na andishi na maathiriano ya fasihi andishi na simulizi. imebainika kwamba waandishi wengine huathiriwa kifani, kimaudhi na kidhamira. Katika sura hii imebainika kwamba fasihi andishi haijavumbua dhamira mpya. Pia imebainika kwamba michezo mingi ya redio ambayo hupendwa sana na wasikilizaji ni fasihi simulizi. Utafika ulidhamiria kuhakiki jinsi fasihi simulizi inavyoiathiri tamthilia ya kiswahili katika kutumia masimulizi na malumbano kama mtindo wa uandishi. Sura ya tatu imechunguza jinsi wa masimulizi ulivyotumiwa katika tamthilia ya kiswahili. Pia sura hii imejadili historia fupi za waandishi wa tamthilia za wingu jeusi na pango ambao ni chacha na wamitila. Vile vile mihtasiri ya tamthilia za wingu jeusi na pango imeonyeshwa ili kumpa mtafiti mwelekeo kuhusu falsafa ya waandishi hawa. Sura ya nne imechunguza matumizi ya mtindo wa malumbano katika tamthilia za wingu jeusi na pango. Utafiti umebainisha kwamba malumbano huweza kusababishwa na maswala ya kijamii, kisiasa,kiuchumi,kidini na kadhalika. Pia imebainika kwamba malumbano huweza kuwa na athari hasi kama vile kukasirika,kutukanana,kudharauliana na kadhalika. Sura ya tano imejadili muhtasari wa utafiti huu. Pia imeonyesha matokeo ya utafiti, matatizo ya utafiti, mchango wa utafiti huu na mapendekezo ya mtafiti. Mwishowe kuna marejeleo ya utafiti huu. Utafiti huu pia ni miongoni mwa kazi chache ambazo zimewahi kuhakiki tamthilia za wingu jeusi na pango kwa kuzihusisha na vipera vya fasihi simulizi na pia kuzihakiki kwa kuzingatia nadhria mseto za uhakiki wa kimtindo na mwingilianomatini. Utafiti huu utawasaidia wahadhiri na wanafunzi wa vyuo vikuu,n pia wanafunzi wa shule za upili,kwani somo la kiswahili linahusisha fasihi simulizi na andishi. Pia mtafiti anaamini kwamba utafiti huu utawafaidia wapenzi wote wa lugha ya kiswahili.
Description
Abstract
Department of Education,217p.The PL 8704 .M85M3 2010
Keywords
hacha, Chacha Nyaigoti's Wingu jeusi --History and criticism, Wamitila, Kyalo Wadi's Pango --History and criticism, Swahili drama --Kenya
Citation