Mielekeo ya Wauza Mifugo Mnadani Wanaozungumza Kinandi Kuhusu Kiswahilikatika Kaunti ya Nandi

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorJepkemboi ,Anne
dc.date.accessioned2026-02-05T10:00:34Z
dc.date.available2026-02-05T10:00:34Z
dc.date.issued2025-11
dc.descriptionTasnifu hii Imewasilishwa Katika Idara ya Kiswahili Ili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili Katika Chuo Kikuu cha Kenyatta msimamizi Jacktone Onyango
dc.description.abstractUtafiti huu ulilenga kueleza jinsi mielekeo ya wauza mifugo mnadani katika kaunti ya Nandi kuhusu lugha ya Kiswahili inavyoathiri matumizi yao ya lugha. Mwelekeo wa watu kuhusu vitu au dhana unaweza kuathiri wale watu au dhana hizo. Tafiti tofauti zilizofanywa kuhusu mielekeo ya watu kwa lugha zimebaini kuwa mielekeo ya watu huweza kuwa hasi au chanya kutegemea masiala mbalimbali kama vile elimu, umri, mazingira, jinsia na kadhalika. Utafiti huu uliongozwa na malengo yafuatayo: kupambanua mielekeo ya wauza mifugo mnadani wanaozungumza Kinandi kwa lugha ya Kiswahili katika kaunti ya Nandi; kubainisha mambo ambayo husababisha mielekeo ya wauza mifugo mnadani wanaozungumza Kinandi kuhusu lugha ya Kiswahili na kuchunguza athari ya mielekeo hiyo ya lugha kwa maendeleo ya Kiswahili katika jamii hii. Nadharia ya Utendaji Razini (Theory of Reasoned Action) iliyoasisiwa na Fishbein na Ajzen (1975) ilitumiwa kuongoza utafiti huu. Wataalamu hawa wanasema kuwa binadamu ni viumbe wanaofikiria na wanajua aina ya mielekeo na tabia walizo nazo. Kwa hivyo, maelezo ya watafiti hawa yanalingana na lengo la utafiti huu ambalo ni kueleza matumizi ya Kiswahili miongoni mwa wauza mifugo mnadani ambao mielekeo yao hudhihirika kupitia matumizi yao ya lugha. Utafiti huu ulihusisha wauza mifugo 35 kutoka minada yote 7 katika kaunti ya Nandi. Mtafiti alitumia idadi hii kimaksudi. Utafiti huu ulitumia mbinu ya utafiti wa maelezo ambapo data ilikusanywa kupitia hojaji, mahojiano na kushiriki utendaji kisha ikachanganuliwa na kuwasilishwa kupitia majedwali, baa grafu na pai chati. Ilibainika kwamba wauza mifugo mnadani wana mitazamo hasi kuhusu utumiaji wa Kiswahili kwa sababu wanahisi Kiswahili ni kigumu kwao. Matokeo ya utafiti huu yanaweza kutumiwa na washikadau mbalimbali wanaohusika na lugha ili kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa Wakenya wote wanafahamu na kutumia kwa ufasaha lugha ya Kiswahili ili wabadili mielekeo yao hasi kuhusu lugha hii.
dc.identifier.urihttps://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/32286
dc.language.isoother
dc.publisherKenyatta University
dc.titleMielekeo ya Wauza Mifugo Mnadani Wanaozungumza Kinandi Kuhusu Kiswahilikatika Kaunti ya Nandi
dc.typeThesis
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Full-text Master Project.pdf
Size:
1.68 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
2.66 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: