Mtindo kwenye Nyimbo za Jadi Katika Jamii Ya Wakisii Na Waswahili wa Nchini Kenya
Loading...
Date
2025-06
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Mtindo ni uti wa mgongo katika tungo za kisanaa, iwe hadithi, tamthilia, ushairi na hata nyimbo. Utafiti huu umejikita katika kuhakiki mtindo kwenye nyimbo za jadi za jamii ya Wakisii na jamii ya Waswahili wa nchini Kenya. Watafiti mbalimbali wametafiti swala la mtindo katika nyimbo kama vile: Iyaya na wenzake (2021) walitafiti mtindo na lugha ya uwasilishaji katika nyimbo za nyiso za jamii ya Watachoni ambazo ni wenyeji wa Kenya. Muriuki (2013) alitafiti mtindo katika nyimbo za kazi katika jamii ya Warabai. Utafiti huu unatofautiana na tafiti za hapo awali hasa kwa msingi wa malengo na mambo mengine. Utafiti huu umefanikiwa katika: kubainisha jinsi ambavyo watunzi wametumia mbinu za mtindo katika kusawiri historian a tamaduni za jamii ya Wakisii na Waswahili wa nchini Kenya. Hali kadhalika, utafiti huu umehakiki mbinu za mtindo kwenye nyimbo za jadi za jamii ya Wakisii na Waswahili. Mwisho kabisa, utafiti huu umefanikiwa kuchunguza jinsi ambavyo mbinu za mtindo zilivyotumiwa kufanikisha uwasilishaji wa maudhui katika jamii teule. Nadharia ya mtindo ambayo iliasisiwa na Coombes ndiyo iliongoza utafiti huu. Coombes (1953) anasema kuwa mtindo huchunguza lugha na kanuni zinazoongoza lugha yenyewe ili kubainisha mbinu za kimtindo zilizotumiwa, sababu ya mbinu hizo kutumiwa na athari ya mbinu hizo katika kazi husika. Katika nadharia hii lazima mhakiki wa kazi yoyote ile ya fasihi achunguze vipengele hivyo na aelewe utendekazi wake. Waitifaki wengine ni kama Leech na Short (1981) ambapo wanasema kuwa nadharia hii ina lengo la kuelezea uhusiano uliopo baina ya lugha na majukumu ya kisanaa. Ambapo swali kuu ni mbona mwandishi akaamua kujieleza kwa njia fulani? Nyimbo za jadi za jamii ya Wakisii na Waswahili zilizotumiwa katika utafiti ziliteuliwa kwa kutumia mbinu ya maksudi ambapo nyimbo zenye ukwasi wa mtindo ndizo zilizingatiwa. Utafiti hulifanywa makatabni na nyanjani. Maktabani ulihusisha kusoma vitabu, tasnifu, matini na majaida kuhusu mtindo. Nyanjani ulijumuhisha kuwahoji watu kumi wakongwe kutoka kila jamii na kila jinsia ikiwakilishwa na watu watano watano. Hali kadhalika, hadhira ambayo ilishiriki katika uimbaji isailiwa ambapo watu wawili wawili kutoka kila sherehe walishirikishwa na mwisho kabisa watu wanne kutoka kila jamii ambao waliongozwa katika uimbaji wa nyimbo hizo walishirikishwa katika utafiti. Wawili wawili kutoka kwa kila jinsia. Mbali na hayo, mbinu ya kusikiliza na kurekodi nyimbo hio za jadi ilitumiwa baada ya hapo uchambuzi ukaanza. Data ilichanganuliwa kwa kuongozwa na mihimili ya nadharia, maswali na malengo ya utafiti. Kazi hii imepangwa katika sura tano. Utafiti huu uliweza kubainisha kuwa mbinu za mtindo zina nafasi kubwa katika kuendeleza nyimbo za jadi. Utafiti huu utakuwa na mchango mkubwa katika uwanaja wa fasihi simulizi kwa utawasadia wataalamu wa fasihi nawanafunzi wa fasihi kuchanganua na kuelewa mtindo katika nyimbo za jadi za jamii husika na pia katika kuhakiki mtindo katika tanzu zingine za fasihi simulizi.
Description
Tasnifu hii Imetolewa ili Kutosheleza baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili ya Chuo Kikuu cha Kenyatta, June 2025.
Msimamizi
Joseph Jesse Muriithi