Historia na Bunilizi katika Kaburi bila Msalabana Wimbo Mpya

Loading...
Thumbnail Image
Date
2023-03
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulichunguza uhusiano uliopo kati ya historia na bunilizi katika riwaya za Kaburi Bila Msalaba (Karcithi, 1969) na Wimbo Mpya (Mbatiah, 2004). Riwaya hizi zina mchango thabiti kwa bunilizi na historia. Hoja hizi thabiti hazijafanyiwa utafiti wa kina. Utafiti huu ulitumia vigezo vya matukio, usawiri wa wahusika na mitindo katika viwango mbalimbali ili kufikia malengo yake. Utafiti huu uliongozwa na malengo yafuatayo; Kwanza, kuchambua maudhui ya kihistoria na kibunilizi katika riwaya za Kaburi Bila Msalaba na Wimbo Mpya. Pili, kuchunguza usawiri wa wahusika wa kihistoria na wa kibunilizi katika riwaya za Kaburi Bila Msalaba na Wimbo Mpya. Tatu, kubainisha jinsi vipengele vya kibunilizi vilivyotumika katika riwaya za Kaburi Bila Msalaba na Wimbo Mpya. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uhalisia wa Kihistoria. Kwa kuzingatia mihimili ya nadharia hii, riwaya teule zilihakikiwa ili kupata matokeo yaliyotosheleza mabhitaji ya utafiti. Data ilirckodiwa na kuchanganuliwa kulingana na malengo ya utafiti, maswali ya utafiti na mihimili ya nadharia husika. Matokeo yaliwasilishwa kwa njia ya maclezo. Mbinu za utafiti zilijumlisha; Muundo wa utafiti, mahali pa utafiti, uteuzi wa sampuli, ukusanyaji wa data, uchanganuzi wa data na uwasilishaji wa matokeo. Kutokana na utafiti huu mahsusi, tulipata kuwa riwaya teule zina viwango mbalimbali vya kihistoria na kibunilizi. Hivyo basi ilibainika kuwa bunilizi na historia vinakuwa vigezo muhimu vya kuendeleza fasihi kwa mujibu wa utafiti huu.
Description
Tasnifu Hii Imetolewa ili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaii ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Machi 2023. Wasimamizi Richard Wafula Ngugi Boniface
Keywords
Citation