Ubora wa tafsiri katika kamusi tafsiri za mtandaoni

Loading...
Thumbnail Image
Date
2024-06
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Kiswahili ni lugha inayozidi kukita mizizi kidijitali kupitia mbinu anuai ikiwemo programu za kamusi na vitabu vingine kama Bibilia vilivyoswahilishwa na kuhifadhiwa mtandaoni. Utafiti huu ulinuia kudihirisha ubora wa tafsiri ya maneno yaliyotolewa katika kamusi-tafsiri za mtandaoni. Kwa kuwa enzi hii kuna watumizi wengi wa mtandao kwa malengo anuai, kamusi za mtandaoni zina dhima kuu na hivyo kuwepo na tafsiri potovu kunaweza kuwaathiri watumiaji wengi. Utafiti ulichukua muundo wa kutathmini tafsiri ya maneno kwenye kamusi zilizoteuliwa za mtandaoni kuanzia alfabeti A – M na kutoa mapendekezo ya tafsiri bora zaidi, kwa msaada wa wataalamu wa lugha kama vile waandishi wa kamusi kama walivyolengwa na mtafiti. Mtafiti alishirikiana moja kwa moja na wataalamu hawa kama vile waandishi wa vitabu mbalimbali na wanaotumia kamusi hizi katika kuandaa tasnifu yake kupitia kwa mahojiano, hojaji pamoja na mawasiliano ya kila mara kupitia simuni ili kuhakikisha kuwa malengo yake yametimia. Utafiti huu ulilenga tafsiri ya Kiingereza-Kiswahili na wala sio lugha zingine. Mihimili ya Nadharia ya Isimu Kongoo ilitumika katika kupendekeza kongoo matini bora inayotumika kama tafsiri kwa kamusi za mtandao. Mbali na nadharia hii, nadharia ya Ulinganifu wa Kimuundo ambayo ni mojawapo ya miavuli ya nadharia ya Tafsiri ilitumika katika kuasisi tafsiri bora kwa maneno. Utafiti ulikuwa wa kimaelezo, na usampulishaji wa kimakusudi ulitumika katika kuwateua wahojiwa pamoja na kuteua data kutoka kwenye kamusi za mtandao. Data ilichanganuliwa kwa mwongozo wa mihimili ya nadharia pamoja na malengo ya utafiti. Baada ya kuchanganua data, matokeo yaliwasilishwa kwa kutumia maelezo na michoro ya jadwali kisha kutolewa maelezo yake. Matokeo ya utafiti yananuia kuboresha tafsiri ya kamusi kwenye mtandao ili kuwafaidi wategemezi, waunfaji na watumiaji wa kamusi hizi katika shughuli zao anuai. Baadhi ya watakaoweza kufaidi kwa kamusi yenye tafsiri bora ni pamoja na wasomi, watafsiri, walimu, pamoja na wageni wanaotumia kamusi hizi ili kujifundishia lugha ya Kiswahili.
Description
Katika kutimiza baadhi ya mahitaji ya shahada ya Uzamili katika chuo kikuu cha kenyatta Juni 2024
Keywords
Citation