Usawiri wa Wahusika wa Kiume katika Riwaya za Kiswahili Zilizoandikwa na Wanawake

Loading...
Thumbnail Image
Date
2022
Authors
Kanwa, Olivia
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulishughulikia usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya za Kiswahili zilizoandikwa na wanawake. Utafiti umechunguza kazi za waandishi wa kike wa Kenya na wa Tanzania kwa kutumia mkabala linganishi. Malengo manne ya utafiti huu ni: kubainisha dhamira zinazowasilishwa na wahusika wa kiume, kuchanganua taswira zinazotumiwa na waandishi kuwasawiri wahusika wa kiume, kujadili mitazamo inayoibuliwa na wahusika wa kiume katika riwaya teule na kulinganisha na kulinganua waandishi wakike wa Kenya na Tanzania katika usawiri wao wa wahusika wa kiume. Riwaya mbili za waandishi wa kike wa Kenya ni Tumaini iliyoandikwa na Clara Momanyi, Dago wa Munje iliyoandikwa na Sheilla Ryanga na za kutoka Tanzania ni Kipimo cha Mizani ya Zainabu Burhani, Hiba ya Wivu ya Zainabu Mwanga zilihakikiwa kwa kufuata utaratibu. Sanjari na hilo, tasnifu hii imeonesha kuwa nadharia ya uhalisia, ujifunzaji wa kijamii (imejikita kwenye uana) na mwanaume mpya zimekuwa nadharia faafu zilizoongoza utafiti huu. Uhalisia umefafanuliwa kama msingi wa usawiri katika jamii kwa maana hutofautiana kulingana na hali na baina ya jamii moja na nyingine. Nadharia ya ujifunzaji wa kijamii huona tabia kama kitendo ambacho mtu hujifunza kutoka katika mazingira ambayo ndiyo hupelekea umuhimu wa majukumu ya kiuana. Mwisho, utafiti ulitumia nadharia ya mwanaume mpya, nadharia inayojaribu kuelezea kwanini baadhi ya wanaume hukaa na wake zao kwa usawa bila tabia za mfumo dume ambazo huashiria kuwepo kwa taasubi ya kuumeni. Nadharia hizi tatu zilitumika kujibu sehemu mbalimbali za maswali ya utafiti. Mbinu za utafiti zilizotumika ni usomaji wa riwaya teule kwa kina na kuhakiki. Kutokana na uhakiki, wahusika wa kiume wamesawiriwa chanya na waandishi wanawake. Wachache walikuwa hasi. Wameonesha pande mbili za wahusika kwa kuwachora hasi na chanya. Utafiti huu umesaidia kuongeza maarifa katika eneo la kijinsia na tahakiki za kifasihi.
Description
Tasnifu hii Imewasilishwa ili Kutosheleza baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamifu katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Mei, 2022
Keywords
Usawiri, Wahusika, Kiume, Riwaya za Kiswahili, Zilizoandikwa, Wanawake
Citation