Fasihi Yakiswahiliya Watoto: Maendeleo, Nadharia, Mbinu na Mifano: va Uchambuzi

dc.contributor.authorNgugi, Pamela M.Y.
dc.contributor.authorLyimo, Edlth B
dc.contributor.authorBakize, Leoard H.
dc.date.accessioned2024-02-09T07:16:24Z
dc.date.available2024-02-09T07:16:24Z
dc.date.issued2019
dc.descriptionBook Chapteren_US
dc.description.sponsorshipKitabu hiki, ambacho ni cha kwanza katika Fasihi ya Kiswahili ya Watoto, kina sehemu kuu nne zinazoundwa na jumla ya sura kumi na moja. Mgawanyo huo umefanywa ili kumwezesha msomaji kusoma kwa mtiririko mzuri na pia kumrahisishia kupata maarifa kwa mfuatano unaohusiana na kuathiriana. Kila sehemu ya kitabu hiki imebeba sura kadhaa ambazo zinaisheheneza na kuipa sehemu husika maarifa stahiki. Katika sehemu ya kwanza, yenye jina "Fasihi ya Watoto na Nadharia za Ukuaji," tumetoa maarifa ambayo tunaweza kuyabebesha jukumu la usuli. Sehemu hii inamakinika na kububujisha maarifa tangulizi ambayo kwa pamoja yanalenga kumtambulisha msomaji katika uga wa fasihi ya watoto ya Kiswahili ili iwe rahisi kwake kuelewa hoja na maarifa mengine yatakayotolewa katika sehemu na sura zitakazofuata. Sehemu hii ya kwanza ina sura mbili ambazo zinahusiana. Katika sura ya kwanza tumeifafanua kwa kina dhana ya fasihi ya watoto kwa ujumla pamoja na sifa za fasihi hiyo. Aidha, katika sura ya pili tumefafanua nadharia mbalimbali za ukuaji wa watoto. Lengo hasa ni kujaribu kuwaelewa watoto kwa map ana ili msomaji aelewe vizuri kazi za fasihi ambazo zinawafaa watoto kulingana na viwango vyao vya makuzi na mazingira yao kijamii. Sehemu ya pili ya kitabu hiki inamakinika na "Fasihi ya Watoto na Kumbo zake." Kama ilivyo fasihi ya watu wazima au fasihi kwa ujurnla, fasihi ya watoto nayo ina kumbo kadhaa ambapo msomaji analazimika kuzifahamu ili iwe rahisi kuzielewa na kuzichambua. Sehemu hii .nayo ina sura mbili. Katika sura ya tatu tumezama kwa xx kina katika kufafanua na kujadili kumbo za fasihi simulizi ya watoto. Tena, katika sura ya nne tumemalizia kwa kufafanua kumbo za fasihi ya watoto kwa kuangazia kumbo mbalimbali za fasihi andishi zinazowahusu watoto. Katika sehemu ya tatu tumeangazia "Maendeleo na Wadau wa Fasihi ya Kiswahili ya Watoto." Sehemu hii ina sura nne. Ndani ya sura ya tano tumeangazia maendeleo ya fasihi ya watoto nchini Tanzania na Kenya. Tumefanya hivyo kwa sababu tafiti nyingi za fasihi ya watoto zinakiri kwamba nchi hizo mbili ndizo kitovu hasa cha fasihi hii. Katika sura ya sita tumeainisha wadau mbalimbali ambao wanahusika moja kwa moja na kazi za watoto. Lengo hasa ni kutaka kumfanya msomaji aelewe namna ambavyo wad au hao wanaiendeleza au kuidurnaza fasihi hii ya watoto. Miongoni mwa wadau wa fasihi ya watoto, taasisi nazo hazikubaki nyurna. Hivyo, sura ya saba inaangazia Mradi wa Vitabu vya Watoto nchini Tanzania na mchango wake katika kuendeleza uga huu. Tena, katika sura ya nane, turneizungumzia TATAKI na mchango wake katika kuukuza uga huu wa fasihi ya watoto ndani na nje ya Tanzania. Sehemu ya nne imejikita katika "Ucharnbuzi na Tafsiri katika Fasihi ya Watoto." Baada ya kupata maarifa ya kutosha katika sura zilizotangulia, sehemu hii inarnzamisha msomaji katika kuangalia walau mifano kadhaa ya ucharnbuzi wa kazi za fasihi ya watoto. Katika kulitimiza hili, katika sura ya tisa, tumezungurnzia watoto na ucharnbuzi wa fasihi yao. Katika sura hiyo tumeeleza kwa kina na kujenga hoja kwamba, ingawa uhakiki mwingi wa kazi za watoto unafanywa na watu wazima, lakini kuna umuhimu wa kuwaingiza watoto wenyewe katika ulimwengu wa uhakiki wa kazi zao. Hii inaweza kuleta upya wa vionjo vya ucharnbuzi. Vionjo hivi vitaiparnba fasihi na kuisheheneza maarifa halisi arnbayo yanaweza kuonesha kwarnba watu wazima hawaimiliki fasihi ya watoto wao bali wanawasaidia pia watoto katika kucharnbua fasihi yao. Katika sura ya kurni tumetoa mfano wa uchambuzi wa kazi za watoto kwa kujikita katika masuala ya ujinsia katika fasihi ya watoto ya Kiswahili. Hatimaye, katika sura ya kumi na moja, tumeangazia masuala ya usilimishaji na tafsiri katika fasihi ya watoto. Katika sura hii tumeonesha kwa undani kwamba kazi za watoto si lazima ziwe zile zinazotokana na watoto wajamii moja tu. Wakati mwingine kazi za watoto zajamii moja zinaweza kusilimishwa au kutafsiriwa na hatimaye zikawafaa watoto wa jamii nyingine mbali na jamii ile iliyoandikiwa mwanzo.en_US
dc.identifier.issn9789976531695
dc.identifier.urihttps://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/27615
dc.language.isootheren_US
dc.publisherTaasisi Ya Taaluma za Kiswahilien_US
dc.titleFasihi Yakiswahiliya Watoto: Maendeleo, Nadharia, Mbinu na Mifano: va Uchambuzien_US
dc.typeBook chapteren_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Fasihi ya Kiswahili ya watoto maendeleo, Nadharia, , binu na ilano va Uchambuzi...pdf
Size:
1.47 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text book chapter
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: