Fasihi ya Watoto kama Njia ya Kukuza Mshikamano wa Kiraifa
dc.contributor.author | Ngugi, Pamela M. Y. | |
dc.date.accessioned | 2024-02-09T07:23:59Z | |
dc.date.available | 2024-02-09T07:23:59Z | |
dc.date.issued | 2019 | |
dc.description | Book Chapter | en_US |
dc.description.abstract | Lengo la nchi yoyote iliyojikomboa kutokana na ukoloni na kupata uhuru ni kugeuza asasi za kiukoloni ilizorithi ili ziweze kuhudumia mahitaji na tamaduni za jamii mpya (Ochieng, 1985 katika Mbatia, 2012). Kenya ilipopata uhuru mwaka wa 1963, na kikwazo kikuu katika ujenzi wa taifa jipya kilikuwa ni ukabila. Wakenya waliendelea kudumisha uaminifu kwa makabila yao kama ilivyokuwa kabla ya ukoloni. Hivyo basi kulikuwa na haja ya kubuni njia za kukabiliana na hali hii. Ujenzi wa utarnbulisho wa kitaifa ni muhimu katika kupunguza migogoro ya kikabila na kimbari. Utambulisho huu hauji kisadfa bali hujengwa kimakusudi kama sehemu ya ajenda ya viongozi wenye mtazamo mpana na urazini wa kitaifa. Kama anavyosisitiza Njogu (2012) "Utambulisho wa kitaifa unasaidia katika kuimarisha asasi za utawala bora, kuwajibisha viongozi na kuweka uwazi katika utoaji huduma kwa umma." Tangu enzi za kabla ya uhuru hadi sasa, Kiswahili kama lingua franka kimeweza kutoa mchango muhimu katika kujenga mshikamano wa kitaifa, (Mbatia, 2012). Kwa mfano, mara tu baada ya uhuru Kiswahili kilichangia katika kujenga tabaka la wafanyikazi ambalo lilijumlisha watu kutoka makabila mbalimbali. Watu waliotoka mashambani na kuja kufanya kazi katika miji mbalimbali walilazimika kutumia Kiswahili ili kuweza kuwasiliana. Hivyo basi lugha ya Kiswahili ikawa mojawapo wa nyenzo za kujenga utaifa wa Kenya. Baada ya uhuru, serikali ya Kenya iliteua TUl11eya Ominde chini ya Uenyekiti wa Prof S.H. Ominde. Jukumu la tume hiyo lilikuwa ni kushauri serikali kuhusu utungaji na utekelezaji wa sera ya elimu baada ya kufanya uchunguzi uliohitajika. Tume hii iliibuka na malengo kadhaa ya elimu nchini Kenya.Lengo mojawapo la elimu lilikuwa na lingali ni kukuza utaifa, uzalendo na kuendeleza umoja wa taifa. Hivyo basi, elimu inayotolewa inahitaji kuziheshimu tamaduni mbalimbali zilizopo nchini na wakati uo huo, kuhakikisha kuwa haiendelezi ubaguzi katikajamii kwa misingi ya rangi, ukabila na dini. IIi kutekeleza lengo hili na malengo mengine, wasomi wengi wanaamini kuwa ufundishaji wa fasihi kwa jumla na hasa fasihi ya watoto unaweza kuchangia katika kuyafikia malengo haya kwa kukuza hisia za kitaifa miongoni mwa wanafunzi. ,- Ujenzi wa taifa ni juhudi za makusudi na za kujitolea. Tangu uhuru, wananchi wamekuwa wakitafuta njia za kuleta utangamano baina ya makabila na nchi mbalimbali za Afrika. Hatua moja kuhusu ujenzi wa taifa ni uimarishaji wa utamaduni wa tamaduni mbalimbali. Utamaduni wowote ule utaeleweka vyema kwa kuchunguza mila na desturi zilipo katika jamii husika, pamoja na kufahamu namna kila jamii ilivyowasilisha amali zake mbalimbali kama vile, ukarimu, kujitolea, haki na maslahi ya pamoja, mambo ambayo yalichangia katika kuunda utaifa. Ufahamu wa amali hizi waweza kupatikana kupitia fasihi za jarnii hizi. Fasihi ni matokeo ya shughuli za jamii; huibuka, hukua na kusambaa kutokana na mazingira yaliyopo katika jamii. Lengo la sura hii ni kubainisha dhima ya fasihi ya watoto kama kichochezi cha kujenga | en_US |
dc.identifier.isbn | 978-9966-133-55-7 | |
dc.identifier.uri | https://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/27616 | |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | Moi University Press, Moi University, Eldoret | en_US |
dc.title | Fasihi ya Watoto kama Njia ya Kukuza Mshikamano wa Kiraifa | en_US |
dc.type | Book chapter | en_US |
Files
Original bundle
1 - 1 of 1
Loading...
- Name:
- Fasihi ya Watoto kama Njia ya Kukuza Mshikamano wa Kiraifa.....pdf
- Size:
- 6.13 MB
- Format:
- Adobe Portable Document Format
- Description:
- Full text book chapter
License bundle
1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
- Name:
- license.txt
- Size:
- 1.71 KB
- Format:
- Item-specific license agreed upon to submission
- Description: