Usawiri wa wanasiasa kama kuwahusika katika makala za habari kwenye gazeti la Taifa Leo nchini Kenya

Loading...
Thumbnail Image
Date
2012-07-06
Authors
Kirichia, J. K.
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu ulilenga kutathimini na kubainisha jinsi ambavyo waandishi wa magazeti hususan lile la Taifa lea huwasawiri wanasiasa kama wahusika katika miktadha maalumu ya kisiasa. Kutokana na udurusu wa kazi mbalimbali zilizofanyiwa utafiti inabainika kwamba swala la kuwasawiri wahusika hao haujashugulikiwa. Tafiti za awali zimehusisha usawiri wa wahusika wa kubuni ilihali utafiti huu umemwangalia mwanasiasa ambaye ni mhusika halisi. Kusudi la utafiti huu lilikuwa ni kuziba pengo la kiusomi kwa kuchunguza kwa uketo j insi ambavyo waandishi wa habari kwenye gazeti la Taifa Leo huwaeleza wahusika wa kisiasa ambao wameteuliwa. Wanasiasa hutekeleza majukumu muhimu katika jamii kwa mfano kutetea hali fulani ambazo si nzuri. Wanasiasa aidha, huchangia kuunda sera ambazo ni muhimu katika ustawi wa nchi. Utafiti huu umemwangazia mwanasiasa kama mhusika na kuonyesha jinsi waandishi wa habari wanavyowaeleza katika makala mahususi katika gazeti la Taifa Leo. Utafiti huu umebainisha kuwa wanasiasa huwa na sifa mbalimbali kutegemea na muktadha wa kisiasa waliomo. Aidha, ni kweli wanasiasa wengine huwa makini kupata sifa nzuri kutoka kwa raia wanaowachagua. Kukiwa na msiba, wao huonekana wenye huruma na hali ikiwa tofauti hudhihirisha sifa tofauti. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ile ya Mtindo na Uamali. Nadharia ya mtindo inaeleza kwamba kazi ya fasihi haiwezi kueleweka bila lugha katika kutoa ujumbe wake kwa wasomaji au wasikilizaji. Nadharia ya uamali nayo hutilia mkazo matumizi ya lugha, watumiaji wake na majukumu ya lugha katika jamii. Sura ya kwanza ambayo ni utangulizi imeshughulikia maswala ya kikaida kwa mujibu wa matakwa ya Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika, Chuo Kikuu cha Kenyatta kama vile swala la utafiti, sababu za kuchagua mada, malengo ya utafiti, misingi ya nadharia, yaliyoandikwa kuhusu mada hii na mbinu za utafiti. Katika sura ya pili mtafiti ameangazia gazeti na wanasiasa. Aidha mwingiliano wa vyombo vya habari na fasihi umeshughulikiwa. Sura ya tatu imewaangazia wahusika wanasiasa walioshughulikiwa, mandhari yao na usawiri wao mtandaoni. Sura ya nne imekuwa ni uchanganuzi wa data kutokana na makala teule ya gazeti la Taifa Leo. Mitindo mbali mbali ya usawiri iliyotumiwa na waandishi wa habari imezingatiwa. Sura ya tano ambayo ni ya mwisho ni hitimisho na matokeo ya utafiti kwa jumla. Pia sura hii imetoa mapendekezo ya utafiti wa baadaye. Isitoshe sura hii imeonyesha changamoto zilizopatikana katika utafiti huu na mwishowe kuonyesha umuhimu wa matokeo ya utafiti. Data ya utafiti huu imekusanywa maktabani na nyanjani na kisha kuchanganuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya kimaelezo kwa kuzingatia mihimili ya nadharia ya uamali na kimtindo.
Description
Department of Kiswahili and African Language: 116p. The P 95.82 .K52 2012
Keywords
Mass media, Political aspects, Kenya, Nairobi, Newspapers, Politicians, In mass media, Politics and government, 2007
Citation