Nafasi ya mshikamano katika kukuza maudhui katika insha za wanafunzi wa kidato cha nne katika Kaunti ya Murang’a

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorOgato, Margaret Moraa
dc.date.accessioned2018-09-19T08:48:24Z
dc.date.available2018-09-19T08:48:24Z
dc.date.issued2018-04
dc.descriptionTasnifu inayowasilishwa kwa madhumuni ya kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu Cha Kenyatta. Aprili, 2018en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulitekelezwa kwa madhumuni ya kuchunguza nafasi ya mshikamano katika kukuza maudhui katika insha za wanafunzi wa shule za upili. Mtafiti alichunguza matatizo yanayohusiana na mshikamano pekee katika insha za wanafunzi wa shule za viwango mbalimbali; wilaya, kaunti na taifa. Wanafunzi lengwa ni wa kidato cha nne wa kaunti ya Murang’a. Kusudi la kuchunguza matatizo yanayohusiana na mshikamano lilikuwa kubainisha chanzo cha matatizo hayo kwa madhumuni ya kupendekeza mbinu mwafaka zinazoweza kutumiwa na walimu pamoja na wanafunzi ili kuimarisha ufunzaji na uandishi wa insha. Nadharia zilizoongoza utafiti huu ni nadharia za Sarufi Zalishi na Sarufi Amilifu Mfumo. Nadharia ya Sarufi Zalishi ilisaidia katika kutathmini ung’amuzi na matumizi ya vipengele vya mshikamano katika insha za wanafunzi. Nadharia ya Sarufi Amilifu Mfumo ilisaidia katika kudondoa na kuchanganua maudhui. Utafiti ulifanyiwa nyanjani pamoja na maktabani. Uteuzi wa sampuli kimakusudi ulitumiwa na shule sita zikachaguliwa. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kuainisha mada tofauti tofauti kulingana na malengo ya utafiti kisha kuwekwa kwenye majedwali na vielelezo. Uchanganuzi ulitumia mihimili ya umilisi na utendaji ya Sarufi Zalishi na ya maana tambuzi, maana husishi na maana matinishi ya nadharia ya SAM. Mahitimisho yalionyesha kuwa matatizo ya mshikamano huathiri ubora wa insha za wanafunzi. Utafiti huu unanuia kuwafaidi wanafunzi, walimu watafiti na watahini.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/18626
dc.language.isoenen_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.titleNafasi ya mshikamano katika kukuza maudhui katika insha za wanafunzi wa kidato cha nne katika Kaunti ya Murang’aen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Nafasi ya mshikamano katika kukuza maudhui katika insha za....pdf
Size:
1.34 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: