Usawiri wa Mandhari Katika Diwani ya Doa
Loading...
Date
2025-06
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulishughulikia usawiri wa mandhari katika katika Diwani ya Doa na jinsi mandhari hayo yamechangia katika uwasilishaji wa ujumbe wa mwandishi. Utafiti huu ulilenga kubainisha jinsi mtunzi alivyotumia aina tofauti za mandhari katika kukamilisha ujumbe wake. Utafiti huu umebainisha wazi mandhari mbalimbali katika diwani ya Doa (2018). Aidha, utafiti hu umedhihihirisha namna mandhari hayo yalivyosawiriwa kwa kuweka wazi umuhimu wake katika kukamilisha ujumbe wa mtunzi. Utafiti huu ulichunguza aina za mandhari katika diwani ya Doa (2018). Nadharia ya Naratolojia ndiyo iliyoongoza utafiti huu. Naratolojia iliyoasisiwa na Genette (1972) na baadaye kuendelezwa na De Jong (2012). Nadharia ya Naratolojia huchunguza sifa za muundo wa usimulizi kwa kugawa vipengele ambavyo huhusiana na simulizi kisha kuzingatia uhusiano na uamilifu baina ya vipengele hivyo. Data iliyotumiwa katika uchunguzi huu ilitoka maktabani na mtandaoni. Kwa maktaba, mtafiti alisoma yale yanayohusiana na mada lengwa yakiwemo tasnifu, majarida na vitabu vinginevyo hasa vinavyo husiana na nadharia husika. Mtandaoni mtafiti alisoma baadhi ya tafiti zinazohusiana na mada teule na yanayohusu utanzu wa ushairi. Sampuli kusudio ni nakala ya diwani ya Doa (2018) ambayo ilikuwa muhimu sana katika utafiti huu. Yaliyotokea katika utafiti huu yametolewa kwa maelezo ya kinathari na utoaji wa mifano. Matokeo ya utafiti huu yamepangwa katika sura tano. Matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kuchangia pakubwa katika fasihi ya Kiswahili hasa utanzu wa ushairi kwa kuonyesha aina za mandhari na nafasi yake katika ukuzaji wa maudhui.
Description
Tasnifu ya Utafiti Imetolewa ili Kutosheleza baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika, Mei 2025.
Msimamizi
1.Edwin Masinde