Uchanganuzi wa Kiisimu katika Mashairi Huru ya Kithaka wa Mberia na ya Kezilahabia

Loading...
Thumbnail Image
Date
2025-06
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu ni kuonyesha jinsi ushairi unavyoweza kuchanganuliwa kiisimu. Tasnifu hii inahusu uhakiki wa kiisimu wa ushairi wa Kiswahili katika mashairi huru ya Kithaka wa Mberia na ya Kezilahabi kwa mtazamo wa nadharia ya Fonolojia Mizani. Utafiti huu umejikita katika diwani teule za watunzi waliotajwa ambazo ni Doa, Msimu wa Tisa, Mvumo wa Helikopta, Kichomi na Karibu Ndani. Uteuzi wa diwani hizi ulifanywa kimakusudi kwa kuwa zina aina data iliyodhamiriwa kuchanganuliwa kiisimu ambayo ilitosheleza mahitaji ya utafiti huu. Mashairi sitini yalihakikiwa kutoka katika diwani teule. Vipengele vya kiisimu vilivyochanganuliwa ni: Aina za sentensi, kipengele cha nafsi na uakifishaji. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Fonolojia Mizani iliyoasisiwa na Liberman (1975) ambayo ina madai kuwa mkazo katika lugha uko katika mfumo wa mfuatano wiani wa kimsonge ambao hupanga silabi, maneno na virai katika sentensi. Tasnifu hii ina sura nne: Sura ya kwanza imeangazia utangulizi unaojumulisha vipengele vifuatavyo: mada, suala la utafiti, maswala ya utafiti, malengo ya utafiti, umuhimu wa utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka ya utafiti, yaliyoandikwa kuhusu mada, misingi ya nadharia, mihimili ya nadharia na mbinu za utafiti. Sura ya pili imeshughulikia vipengele vya kiismu vilivyobainishwa na jinsi vinavyotumika katika kuendeleza kazi ya mashairi huru teule ya Kithaka wa Mberia. Sura ya tatu imebainisha vipengele vya kiisimu na kuonyesha jinsi vilivyotumika katika kuendeleza mashairi huru ya Kezilahabi. Sura ya nne imeshughulikia umuhimu wa vipengele vya kiisimu kisha sura ya tano imeshughulikia muhtasari wa utafiti, matokeo ya utafiti, changamoto za utafiti na mapendekezo ya taifi zaidi. Data iliyotumika katika utafiti huu ilikusanywa kutoka maktabani. Maktabani ndiko usomaji ulifanywaa wa diwani za mashairi teule, tasnifu na vitabu vingine vinavyohusiana na mada ya utafiti na nadharia ya utafiti huu. Uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia mbinu ya uhakiki matini kwa kuongozwa na pengo la utafiti, maswali na malengo ya utafiti na kwa kuongozwa na mihimili ya nadharia ya Fonolojia Mizani. Kwa kufanya hivi, utafiti uligundua kwamba mbinu za kiisimu zinaweza kutumiwa katika uhakiki wa mashairi huru ya Kiswahili.
Description
Tasnifu Hii Imetolewa Kwa Madhumni Ya Kutosheleza Baadhi Ya Mahitaji Ya Uzamili Katika Chuo Kikuu Cha Kenyatta, June 2025. Supervisor Edwin W. Masinde
Keywords
Citation