Majigambo ya Kikuria: mtazamo wa kiisimu

Loading...
Thumbnail Image
Date
2012-04-19
Authors
Chacha, Leonard Mwita
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Tasnifu hii ni tahakiki ya majigambo ya wakuria kwa kutumia mtazamo wa kiisimu. Inakusanya na kuchambua miundo ya nje na ya ndani iliyomo kweny mashairi hayo. Inazo sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi wa katika utafiti wetu ambapo kumezingatiwa somo la utafiti pamoja na madhumuni, sababu za kuchagua mada hiyo na upeo wa utafiti. Hali kadhalika, kumefafanuliwa nadharia za utafiti na kugusia yaliyoandikwa na wengine kuhusu made hii. Pia kumetolewa njia za utafiti ambazo zilitumika katika kazi hii. Baada ya kuweka mipaka ya tasnifu katika sura ya kwanza, kumetolewa maelezo ya kijumla kuwahusu wakuria katika sura ya pili. Mambo yaliyofafanuliwa hapa ni eneo lao la kijiografia, historia yao, shughuli za kitamaduni ambayo yalirutubisha na kuzalisha majigambo. Imebainika kwamba majigambo huwa yamehimiliwa ya kijamii na kitamaduni ambayo yalirutubisha na kuzalisha majigambo. Imebainika kwamba majigambo huwa yamehimiliwa na utamaduni fulani, amali fulani, mfumo fulani wa kiuchumi, na mazingira fulani, amali fulani, mfumo fulani wa kiuchumi, na mazingira fulani . Sura hii imeonyesha kuwa majigambo ni zao la mizingira pamoja na mikatikati ya binadamu ya kuhimili maisha. Pia historia imeyapa mashairi uhai na mwelekeo. Katika sura ya tatu kumefanyika tahakiki ya majina ya majisifu. Kumetolewa maelezo yanayoonyesha namna mbalimbali za kupata majina katika jamii hii na jinsi yaavyotumika kama majina ya majisifu. Imeonyeshwa jinsi majina haya ya majisifu yanavyotumika katika majigambo na ikadhihirika kuwa majina ya majisifu ni vipashio vya kimsingi katika majigambo. Pia majina haya huundwa kwa vipengele mahsusi vya kifonolojia na kimofolojia vinavyopatikana katika lugha ya Kikuria. Tofauti kubwa kati ya majigambo ya Kikuria na mashairi ya Kiswahili iliyojitokeza katika sura hii ni kuwa majigambo huwa na utendaji na hutokea panapo muziki. Sura ya nne imeshughulikia uchanganuzi wa mashairi ya majigambo katika viwango vya kifonolojia, kisintaksia, na kisemantiki ambapo imeoneka kuwa ushairi huu huwa na miundo ya nje na ya ndani. Sura hii imebainisha kuwa majigambo huwa na kanuni za dibaji na hitimisho kama vile katika uteuzi wa Kiswahili. Sura ya tano ni hitimisho la uchanganuzi uliofanywa. Katika sura hii kumetolewa muhtasari wa kazi yote kwa jumla hasa ikilenga matokeo ya uchunguzi, matatizo yaliyomkumba mtafiti, mapendekezo kuhusu kazi yenyewe. Kwa jumla, nadharia za umuundo na semiotiki zimefaa katika kila mojawapo ya sura zilizopititiwa. Jinsi zilivyoingiliano zimewezesha kuoanisha bila shida taalum za fasihi na isimu.
Description
Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya 'Masters of Arts' katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Juni 1997; The PL 8422.C49
Keywords
Swahili language
Citation