Itikadi Kama Chanzo cha Migogoro katika Msimu Wa Vipepeo K.W Wamitila (2006) na Mhanga Nafsi Yangu S.A Mohamed (2013).
Loading...
Date
2025-04
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulishughulikia itikadi kama chanzo cha migogoro katika riwaya ya Msimu wa Vipepeo (2006) yake K.W Wamitila na Mhanga Nafsi Yangu (2013) yake S.A Mohamed. Utafiti huu ulinuia kuonyesha itikadi kama chanzo cha migogoro miongoni mwa wahusika katika riwaya teule. Tafiti tofauti zimefanywa na wataalamu kuhusiana na suala la migogoro katika riwaya ya Kiswahili. Hata hivyo, kadri ya ufahamu wa mtafiti haupo utafiti ambao umeangazia itikadi kama chanzo cha migogoro. Aidha, riwaya teule hazijachambuliwa kwa kuangazia mtazamo huu. Utafiti huu ulinuia kuchanganua itikadi kama chanzo cha migogoro katika riwaya teule, kutathmini athari za migogoro hii katika uwasilishaji wa maudhui na ploti katika riwaya na kujadili suluhu za migogoro hiyo kwa kuangazia riwaya teule. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Hejemonia iliyoasisiwa na mwanafalsafa Antonio Gramsci (1985). Mihimili ya nadharia hii ilikuwa ni, Hejemonia hutegemea makubaliano yaliyopo kati ya watawala na wanaotawaliwa, asasi za kijamii hutumiwa na tabaka tawala kuwapumbaza raia na Hejemonia huendelezwa kupitia kwa tamaduni za jamii husika. Mihimili hii ilimwezesha mtafiti kuichanganua data kwa ukamilifu. Mbinu ya kimaelezo ndiyo iliyotumiwa katika uchanganuzi wa data. Matokeo ya utafiti huu yameafikiana na yaliyotarajiwa katika utafiti huu kwa kudhibitisha kuwa itikadi ndizo chanzo cha baadhi ya migogoro iliyopo katika riwaya teule. Ni wazi kuwa, migogoro ambayo chanzo chake ni itikadi huibua maudhui tofauti na humsaidia mwandishi kuijenga ploti katika kazi yake. Mwisho, baadhi ya migogoro katika riwaya inaweza kusuluhishwa kwa kutumia mbinu tofauti ambazo ziliangaziwa. Matokeo ya utafiti huu yatakuwa ya manufaa kwa wasomi, watafiti na waandishi wa riwaya ya kiswahili kwa kukuza maarifa yao kuhusu suala la migogoro na itikadi za wahusika katika riwaya.
Description
Tasnifu Hii Imetolewa Ili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji Ya Shahada ya Uzamili Katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Aprili, 2025
Supervisor:
1.Muriithi Joseph Jesse