Motifu za Yatima Katika Hadithi Teule za Watoto

dc.contributor.authorSudi, Eunice Njoki
dc.date.accessioned2019-03-27T13:03:55Z
dc.date.available2019-03-27T13:03:55Z
dc.date.issued2018-11
dc.descriptionTasnifu hii Imetolewa Ili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili Katika Chuo Kikuu Cha Kenyatta. Novemba, 2018en_US
dc.description.abstractUtafiti huu umechanganua motifu za yatima katika fasihi andishi ya watoto ukitumia hadithi teule za watoto. Utafiti unalenga kubainisha hali zinazochangia watoto kuwa yatima katika hadithi teule za fasihi ya watoto. Pia, utafiti umewezesha kuelewa changamoto zinazowakumba watoto yatima katika jamii. Vilevile utafiti umenuia kuonyesha jinsi mtoto yatima anavyojiopoa kutokana na changamoto zinazomkumba. Nadharia changamano ya vikale iliyoasisiwa na Northrop Frye (1950-1954) na Nadharia ya Uhalisia iliyoasisiwa na Georg Hegel na kuendelezwa na Lukacs (1972) na Larkin (1977) imetumika katika utafiti huu. Mihimili yake imetumika kama dira ya kuongoza utafiti huu katika kuyaafiki malengo yake. Utafiti unakusudia kuhusisha vitabu teule vilivyoandikwa na waandishi tofauti tofauti. Vitabu ambavyo vimerejelewa ni pamoja na: Mama wa Kambo (Kisovi, 2005), Yatima (Wamitila, 2006) na Mateso ya Johari (Ng’ang’a, 2006). Vitabu hivi vimeteuliwa kwa kutumia mbinu kusudio. Pia, vimeshughulikia mhusika yatima kama kikale na mbinu ya kuwasilisha ujumbe katika fasihi ya watoto. Utafiti umejikita maktabani ambamo vitabu, majarida, magazeti, machapisho na tasnifu mbalimbali zimesomwa ili kuupa msingi utafiti. Data iliyopatikana imechanganuliwa na matokeo yakawasilishwa kwa njia ya maelezo na mifano kutolewa kwa kuzingatia malengo ya utafiti. Muhtasari umefanywa baadaye na kutolewa kimaelezo. Utafiti huu umebaini kuwa yatima hupitia maisha yaliyo na matatizo mengi na ya aina mbalimbali. Hata hivyo, utafiti huu pia umebaini kuwa watoto yatima huweza kujiopoa kutokana na matatizo haya kupitia kwa juhudi zao za kibinafsi kama vile kuiombea hali yao, kukumbana na matatizo haya kwa ujasiri wao na hata kufanya bidii ili kujiopoa na hali hizi ngumu wanazokumbana nazo. Kwenye ngazi ya kijamii, watoto yatima huweza kuopolewa na jamaa na hata marafiki. Hali hizi za maisha pamoja na njia wanazotumia kujiopoa yatima hawa zinaambatana na hali ya maisha kwa mtazamo wa nadharia zilizoongoza utafiti huu. Kutokana na haya yote, utafiti huu umependekeza utafiti zaidi juu ya masuala ya maisha ya watoto yatima kwa kuzingatia aina nyingine za fasihi kama vile ushairi, tamthilia na hata hadithi fupi. Pia, imependekezwa kuwa utafiti zaidi uweze kufanywa kule nyanjani kando na huu uliozingatia utafiti wa maktabani.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/19346
dc.language.isoKiswahilien_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.titleMotifu za Yatima Katika Hadithi Teule za Watotoen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Motifu za Yatima katika Hadithi Teule za Watoto.pdf
Size:
7.29 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
full text
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: