Mielekeo na mtindo wa Shafi Adam Shafi katika riwaya za Kuli na Haini
Loading...
Date
2018-05
Authors
Gathenya, Elizabeth Wambui
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
IKISIRI
Utafiti huu umechanganua mtindo na mielekeo kwa kushughulikia matumizi ya
uchimuzi na ukiushi katika riwaya teule za mwandishi Shafi Adam Shafi. Utafiti
unazingatia riwaya mbili teule za Kuli (1979) na Haini (2003). Uteuzi wa riwaya hizo
ulifanywa kwa kutumia mbinu kusudio kwa kuwa zilidhihirisha mtindo wa
mwandishi kupitia matumizi ya uchimuzi na ukiushi ambazo zingetosheleza mahitaji
ya utafiti huu. Utafiti ulizingatia matumizi ya uchimuzi na ukiushi wa maneno na
maana katika riwaya husika. Aidha, mielekeo ya mwandishi ya kijamii, kiuchumi,
kihistoria na kimapinduzi inajitokeza. Utafiti huu uliongozwa na nadharia
changamano. Nadharia ya Uhalisia wa Kijamaa na nadharia ya Kimtindo. Mihimili ya
nadharia ya Kijamaa ilifaa utafiti huu kwa kuchanganua mazingira na mielekeo ya
mwandishi. Nayo mihimili ya nadharia ya Kimtindo kama alivyoeleza Leech (1969)
ilitumika katika kubainisha aina za ukiushi wa uandishi wa riwaya husika. Mihimili
ya nadharia ya Kimtindo ilimwongoza mtafiti katika ufasiri wa ujumbe wa riwaya
teule. Matokeo ya utafiti yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo ambapo uchanganuzi
ulizingatia mielekeo ya mwandishi, uchimuzi na ukiushi wa msamiati na maana
katika riwaya zote mbili.
Description
Tasnifu hii imetolewa kwa lengo la kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu Cha Kenyatta. Mei, 2018