Uchunguzi wa Jinsi Masuala Ibuka Yalivyoigizwa katika Ngonjera za Kiswahili katika Tamasha za Drama za Kitaifa Nchini Kenya (2010 – 2017)

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriamen_US
dc.contributor.advisorKitula King‟eien_US
dc.contributor.advisorJessee Murithien_US
dc.contributor.authorYovo, Philomenah Ndinda
dc.date.accessioned2022-03-30T11:21:46Z
dc.date.available2022-03-30T11:21:46Z
dc.date.issued2021
dc.descriptionTasnifu hii Imetolewa ili Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Novemba, 2021en_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulichunguza jinsi masuala ibuka yalivyoigizwa katika ngonjera za Kiswahili zilizoigizwa katika tamashaza drama za kitaifa nchini Kenya (2010 - 2017). Utafiti huu ulikuwa na malengo yafuatayo: kubainisha masuala ibuka yaliyoigizwa katika ngonjera za Kiswahili katika tamasha za drama za kitaifa nchini Kenya (2010–2017), kueleza mbinu za lugha zililizotumika kufanikisha uigizaji wa masuala ibuka katika ngonjera za Kiswahili katika tamasha za drama za kitaifa nchini Kenya (2010 - 2017); na kuchunguza changamoto zilizokumba uigizaji wa masuala ibuka katika ngonjera za Kiswahili katika tamasha za drama za kitaifa nchini Kenya (2010 - 2017). Utafiti ulinuiwa kuonyesha ufanifu wa ngonjera za tamasha za drama kama chombo cha kuwasilisha masuala ibuka na kuelimisha jamii. Sampuli ya ripoti nne za waamuzi wa tamasha za drama (2011, 2012, 2014 na 2015); na kanda nane za ngonjera za tamasha (moja kwa kila mwaka: 2010 - 2017) iliteuliwa kimakusudi kutoka kwa makavazi ya KICD jijini Nairobi kwa idhini ya Taasisi ya Elimu na ofisi ya KNDF nchini Kenya. Data ya maneno na kauli za waigizaji ilikusanywa kwa kusikiza, kutazama na kunukuu ngonjera teule kimaandishi. Vipengele vilivyochanganuliwa kwa kila ngonjera ni masuala ibuka na mbinu za lugha. Ripoti za waamuzi wa tamasha za drama (2011, 2012, 2014 na 2015) zilisomwa ili kuurutubisha utafiti kuhusu changamoto zilizokumba uigizaji wa masuala ibuka katika ngonjera za tamasha. Utafiti uliongozwa na nadharia ya maigizo ya Turner (1969) iloyoendelezwa na Bauman (1977), Schechner (1988), Fine (1994) na Foley (1995). Nadharia ya maigizo inasisitiza umuhimu wa sifa za maigizo bora katika kuchanganua na kuhakiki maigizo ambazo ni tukio au tendo linaloigizwa, jukwaa, sajili, ujumi katika mawasiliano, mila na tamaduni; na iktisadi ya mawasiliano. Tasnifu na vitabu vilivyohusu uigizaji vilisomwa maktabani ili kuurutubisha utafiti. Data ilichanganuliwa kimaelezo kwa kuzingatia nadharia ya maigizo, maswali na malengo ya utafiti. Data ya utafiti iliwasilishwa kimaelezo kwa ripoti. Utafiti ulibainisha kwamba ngonjera za tamasha za drama (2010–2017) zilifumbata masuala ibuka kama vile utetezi wa haki, uhamaji wa wataalamu, Ruwaza ya Mwaka wa 2030, malezi, elimu na ubaguzi. Iling‟amuliwa kwamba mbinu za taswira, jazanda, takriri, tanakali za sauti, tashihisi, methali, chuku na tashbihi zilihusishwa pakubwa katika kufanikisha uigizaji wa masuala ibuka. Utafiti umependekeza kwamba uigizaji wa masuala ibuka katika tamasha za drama za kitaifa utafitiwe zaidi. Utafiti unaweza kufanywa kuhusu jinsi masuala ibuka yalivyoigizwa katika vipera vingine vya tamasha za drama kama vile ngoma bunifu za kisasa, uigizaji bubu, ucheshi wa jukwaani na masimulizi. Aidha, mada ya utafiti inaweza kutafitiwa upya nyanjani kwa kujumuisha waamuzi wa tamasha za drama, wanakamati wa KNDF, shule na vyuo vilivyohusika tamashani pamoja na wakuu wa Wizara ya Elimu.en_US
dc.description.sponsorshipChuo Kikuu cha Kenyattaen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/23430
dc.language.isootheren_US
dc.publisherKenyatta Universityen_US
dc.subjectUchunguzien_US
dc.subjectJinsi Masuala Ibukaen_US
dc.subjectYalivyoigizwaen_US
dc.subjectNgonjera za Kiswahilien_US
dc.subjectTamashaen_US
dc.subjectDrama za Kitaifaen_US
dc.subjectNchini Kenya (2010 – 2017)en_US
dc.titleUchunguzi wa Jinsi Masuala Ibuka Yalivyoigizwa katika Ngonjera za Kiswahili katika Tamasha za Drama za Kitaifa Nchini Kenya (2010 – 2017)en_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Uchunguzi wa Jinsi Masuala ....pdf
Size:
1.45 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Fultext thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: