Mabadiliko ya kimtindo katika ushairi wa Said A . Mohamed

Loading...
Thumbnail Image
Date
2011-12-21
Authors
Ngolo, Elisha Karisa
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Tasnifu hii imeshughulikia baadhi ya mashairi ya Said A. Mohamed kutoka diwani zake tatu: `Sikate Tamaa(1980), Kina cha Maisha(1984) na Jicho la Ndani( 2002). Inajadili mabadiliko ya kimtindo katika ushairi wake kutoka mashairi ya mapokeo hadi yale ya kisasa kwa minajili ya kufafanua sababu zilizoleta mabadiliko hayo. Mashairi mengi katika Sikate Tamaa na Kina cha Maisha yana umbo la kimapokeo. Hata hivyo, kuna baadhi ambayo hayakufuata kaida za kiarudhi kwa ukamilifu. Kwa mfano, kuna mashairi ambayo hayazingatii urari wa vina na mizani kama inavyohalisi kimapokeo. Licha ya hayo, diwani ya Jicho la Ndani ina tofauti kubwa na zile zingine kwa sababu ina mashairi mengi ya kisasa au huru. Utunzi wa tungo hizi unaonyesha kuwa kuna mabadiliko ya kimtindo katika ushairi wake. Madhumni ya kazi hii yalikuwa ni: kuainisha mabadiliko ya kimtindo kutoka mashairi ya mapokeo hadi mashairi huru; kufafanua mazingira na hali zilizosababisha mabadiliko hayo. Vilevile, tulichambua mashairi ili kuthibitisha kwamba ushairi ya Said A. Mohamed hasa ule tunaoita wa `kati' ni ushairi wa Kiswahili. Mwisho ni kuonyesha jinsi mtindo wa matumizi ya lugha unavyoathiri uwasilishaji wa maudhui. Tasnifu hii iliongozwa na nadharia ya utanzu. Nadharia hii inaeleza kwamba tanzu hukua na kubadilika kulingana na wakati, muktadha, jamii, mazingira na uchumi. Aidha kazi zinazoibuka baada ya zile za awali huwa zimefanana na kutofautiana katika utanzu ule ule. Vile vile utanzu huboreshwa na kazi mpya zinazofuata mitindo ya kazi za awali. Nadharia hii ni muhimu kutokana na kwamba ilitupa mwelekeo wa kufahamu sababu za mwandishi kubadili utanzu: toka mashairi mapokeo hadi mashairi huru.Utafiti huu ulifanywa kwa njia ya usomaji wa vitabu, machapisho, makala na tasnifu zingine kutoka maktabani kwa sababu ni kazi ya kifasihi. Uteuzi wa sampuli ni wa kimaksudi kwa sababu unalenga vitabu mahsusi vya mashairi yanayodhihirisha mabadiliko ya kimtindo. Matokeo ya uchunguzi yamedhihirisha kwamba mabadiliko ya kimtindo katika ushairi wa Said A. Mohamed yametokana na mazingira yaliyomkuza mwandishi hususa historia ya Pemba kwa mkabala wa historia ya ushairi wa Kiswahili. Pili ni ubunifu na tajriba za mtunzi zilizomfanya atunge mashairi mengi hasa mashairi `kati'
Description
Department of Kiswahili,144p.The PL 8704.N44.N3 2011
Keywords
History and criticism, Mohamed, Said Ahmed. Kina cha maisha --History and criticism, Mohamed, Said Ahmed. Jicho la ndani --History and criticism, Swahili
Citation