Usawiri wa maudhui ya ndoa katika ushairi wa Euphrase Kezilahabi na Kithaka Wa Mberia
Loading...
Date
2012-02-21
Authors
Gicuku, Margaret
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia usawiri wa maudhui ya ndoa kama yanavyodhihirika katika ushairi wa Kiswahili. Katika kuendeleza kazi hii, mtafiti ameteua ushairi wa Euphrase Kezilahabi; Kichomi (1974) na wa Kithaka wa Mberia Bara Jingine(2001) na Msimu wa Tisa (2007).
Ndoa ni asasi muhimu na ya kimsingi katika maisha ya binadamu. Ni mojawapo ya asasi zinazohakikisha kukua na kuendelea kwa jamii. Utafiti huu umechochewa na imani kwamba ndoa ina manufaa kwa jamii. Ndiyo msingi wa familia na pia ndiyo hujenga jamii.
Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya umuundo-utekelezi. Nadharia hii hueleza kuwa jamii ni mfumo unaochangiwa na vipengele vyake vyote ili kuleta mshikamano na utangamano. Nadharia hii husisitiza juu ya utekelezaji wa majukumu ya wanajamii ili waendelee kuwa vipengele muhimu vya jamii. Ndoa ni mojawapo ya vipengele vinavyochangia mshikamano huo.
Data ya kimsingi imepatikana maktabani kutokana na kazi teule. Aidha mtafiti amesoma makala, vitabu na tasnifu kupata ujumbe unaohusiana na mada hii. Amezingatia pia mtandao ili kufahamu maswala ibuka yanayohusiana na ndoa. Data imechanganuliwa kwa kuzingatia mihimili ya nadharia iliyoteuliwa na kuwasilishwa kwa njia ya maelezo.
Tasnifu hii imegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza imeshughulikia mada ya utafiti, malengo ya utafiti na pia sababu za kuchagua mada hii vilevile zimejadiliwa, pamoja na udurusu wa maandishi yanayohusu mada ya utafiti pamoja na misingi ya nadharia. Mbinu za utafiti zilizotumika katika utafiti huu pia zimeangaziwa.
Sura ya pili imetalii athari za kijamii katika usawiri wa maudhui ya ndoa katika fasihi andishi ya Kiswahili.
Sura ya tatu imebainisha namna mtunzi E.Kezilahabi alivyosawiri changamoto katika asasi ya ndoa, pamoja na hatua zinazofaa kuzingatiwa kukabiliana na changamoto hizo.
Sura ya nne imebainisha usawiri wa changamoto katika asasi ya ndoa kaina unavyojitokeza katika ushairi wa Kithaka Wa Mberia na namna ya kukabiliana na changamoto hizo.
Sura ya tano ni hitimisho na muhtasari wa sura zote pamoja na matokeo ya utafiti huu.
Mapendekezo ya tafiti za baadaye pia yametolewa.
Description
Department of Kiswahili and African Languages,99p.The PL 8704 .G5U8 2011
Keywords
Kezilahabi, Euphrase. Kichomi --History and criticism | Kithaka wa Mberia. Bara jingine --History and criticism | Kithaka wa Mberia. Msimu wa tisa --History and criticism | Swahili poetry