Matumizi ya mbinu za ufupishaji katika mitandao ya kijamii na atharl zake katika lugha ya Kiswahili

Loading...
Thumbnail Image
Date
2016-04
Authors
Jelimo, Doris
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia suala la matumizi ya mbinu za ufupishaji katika mitandao ya kijamii na athari zake katika lugha ya Kiswahili. Lengo kuu la utafiti huu ni kubainisha mbinu mbalimbali zinazotumika katika kufupisha maneno ya Kiswahili katika mawasiliano ya kimtandao. Katika kufanya hivyo, utafiti huu umechunguza matumizi ya Kiswahili katika mitandao ya kijamii na kuonyesha njia kadhaa ambazo mitandao ya Facebook, Twita na Wikipedia imekuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili .. Kwa kuwa lugha ya mtandao huhusu matumizi ya vifupisho, vifupisho hivyo vimebainishwa na athari zake katika lugha yaKiswahili. Nadharia ambayo imeongoza utafiti huu ni nadharia ya Uchanganuzi Tahakiki Usemi (UTU). Nadharia hii hujaribu kueleza uhusiano uliopo kati ya matukio ya kiusemi, siasa, matini, jamii, na utamaduni unavyoathiriwa na itikadi na vile usemi wenyewe unavyoweza kuathiri matukio katika jamii. Data ya utafiti huu ilipatikana kwenye maktaba na mtandao. Mtafiti ametumia njia ya kimakusudi na sampuli kolezi ili kufikia malengo ya utafiti huu. Data ya utafiti irnekusanywa kutoka kwa mitandao mitatu ya kijamii; Facebook, Twita na Wikipedia hasa kwa kuzingatia ujumbe ulioandikwa. Tumekusanya matini ambayo yameandikwa katika lugha ya Kiswahili na hasa yale ambayo yamefupishwa. Matini yaliyokusanywa ni yale ambayo watumiaji wake wametumia mbinu ya akronimu, ufupishaji, kubadilisha na kuchanganya msimbo. Data imechanganuliwa kwa kuzingatia maswali, malengo ya utafiti na mihimili ya nadharia ya Uchanganuzi Tahakiki Usemi. Uchanganuzi wa data ulizingatia hatua tatu kutegemea malengo ya utafiti. Data ya utafiti huu imewasilishwa kwa njia ya kimaelezo na kwa kutolea mifano katika majedwali. Data iliyochanganuliwa imewekwa katika sura tano tofauti hasa kulingana na maswali na malengo ya utafiti. Maelezo toshelevu yarnejumuisha utangulizi na mahitimisho ya kila sura. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa vifupisho vinatumika sana katika mawasiliano ya kimtandao. Jambo hili haliwezi kuepukika wakati huu wa maendeleo ya Ki- TEKNOHAMA. Kwa hivyo, utafiti huu umechangia kuweka wazi matumizi ya Kiswahili katika mitandao ya kijamii. Pia, utafiti umefafanua namna ya kutumikiza vifupisho katika lugha ya Kiswahili kwenye mitandao ya kijamii. Kwa kufanya hivi, utafiti huu umeonyesha kuwa pana haja ya kubuni kamusi za vifupisho vya lugha ya Kiswahili ambavyo vitatumika katika kutoa mwongozo wa mawasiliano kwenye mitandao ya kijamii. Mwisho, licha ya athari za vifupisho ambazo zimeainishwa katika utafiti huu, mbinu za kukabiliana na athari hizi zimefafanuliwa Hi kuendeleza na kukuza lugha sanifu ya Kiswahili katika ulimwengu wa uvumbuzi wa ki- TEKNOHAMA.
Description
Tasnifu hii imetolewa kwa madhumuni ya kutosheleza baadid ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika idara ya kiswahili chuo Kenyatta University. Aprili,2016
Keywords
Citation