Usawiri wa maswala-ibuka katika hadithi za watoto

dc.contributor.authorKaranja, Dorcas Wanjiku
dc.date.accessioned2012-07-24T08:20:19Z
dc.date.available2012-07-24T08:20:19Z
dc.date.issued2012-07-24
dc.descriptionDepartment of Kiswahili and African Languages Department: 135p. The PL 8702 .K37 2012
dc.description.abstractTasnifu hii inajadili usawiri wa maswala-ibuka katika hadithi za watoto. Vitabu vya hadithi vilivyoteuliwa ni miongoni mwa vile ambavyo vimependekezwa na Tume ya Elimu nchini Kenya, visomwe na wanafunzi wa darasa la nne hadi la nane katika shule za msingi, na vivyo ni 'Mnyama mwenye Huruma (2005) na Rebecca Nandwa, 'Ndoto ya Riziki' (2005) na Razwana Kimutai., 'Mama wa Kambo' (2005) na Catherine Kisovi,'Yalianza kimchezomchezo' (2000) na Angelina Mdari, 'Mchuuzi wa matambara' (2006) na Edward Were na 'Ngano za mfalme Tapwara Tapwara'. Nadharia iliyotumika ni ile ya kimtindo na ile yauhalisia. Mihimili ya nadharia hizi ilitumika kama dira ya kuuongoza utafiti huu katika kuyaafiki malengo yake. Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kuainisha maswala-ibuka katika vitabu vya hadithi vya watoto vilivyoteuliwa, lengo la pili lilikuwa ni kuonyesha mitindo iliyotumiwa na waandishi katika kuyasawiri maswala-ibuka na mwisho kabisa utafiti huu ulilenga kutathmini ufaafu wa mitindo hii katika fasihi ya watoto. Data iliyotumika katika utafiti huu, ilikusanywa maktabani ambapo mapitio ya vitabu, majarida, magazeti na tasnifu, yalisaidia katika kuupa msingi utafiti huu, kinadharia na kimpangilio wa data. Data iliyopatikana ilichanganuliwa. Matokeo yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Tasnifu hii ina jumla ya sura tano. Utafiti umeonyesha kuwa waandishi wa fasihi ya watoto wamefaulu katika kuangazia maswala-ibuka katika kazi hizi. Aidha mitindo iliyotumika inafaa na inaafiki kiwango cha watoto.en_US
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/5371
dc.language.isoenen_US
dc.subjectSwahili language
dc.subjectGrammar
dc.subjectStudy and teaching
dc.titleUsawiri wa maswala-ibuka katika hadithi za watotoen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Usawiri wa maswala ibuka katika....pdf
Size:
65.88 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full text thesis
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
2.68 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: