Muundo wa Njeo Katika Lugha ya Kingoni

dc.contributor.advisorChacha, L. M.
dc.contributor.advisorMudhune, E.
dc.contributor.authorHaule, Festo Christantus
dc.date.accessioned2013-12-17T11:41:14Z
dc.date.available2013-12-17T11:41:14Z
dc.date.issued2013-12-17
dc.descriptionPL 8701 .H31
dc.description.abstractUtafiti huu umehusika kuchunguza muundo wa njeo na halinjeo katika lugha ya Kingoni. Mofimu ya njeo na halinjeo katika vitenzi vya lugha ya Kingoni inaundwa kupitia viambishi (mofimu) na toni. Kwa hivyo, masuala matatu ya msingi yameshughulikiwa ili kuweza kubaini muundo wa mofimu hizo. Kwanza, utafiti huu umechunguza viambishi katika vitenzi ili kuvibaini na kuona jinsi vinavyohusika katika kuunda njeo na halinjeo. Pili, umechunguza toni ili kuweza kubaini mwenendo wake katika kuunda njeo na halinjeo katika vitenzi vya lugha hii. Hatimaye, uhusiano wa viambishi na toni katika kuunda njeo na halinjeo za Kingoni umechunguzwa na kubainishwa. Misingi ya Nadharia ya Fonolojia Vipambasauti ambayo inahusika katika uchanganuzi wa toni hususan katika vitenzi na Nadharia ya Fonolojia ya Konsonanti Vokali ambayo inahusika katika uchunguzi wa silabi zimetumiwa. Nadharia hizo zimetumiwa ili kufanikisha malengo ya utafiti huu. Data ya utafiti huu hasa ilipatikana nyanjani ambako vitenzi vya njeo (pia virai tenzi na sentensi kwa ajili ya kubaini halinjeo) viliweza kukusanywa. Data hiyo ilipatikana katika vijiji vitano vya wilaya ya Songea Vijijini ambako lugha ya Kingoni inatumiwa zaidi. Vijiji hivyo ni Mpitimbi, Namatuhi, Matimila, Magagula na Peramiho (mji mdogo). Utafiti huu umegawanywa katika sura tano; Sura ya kwanza inahusu utangulizi wa kazi nzima. Katika kufanya hivyo kiini cha utafiti huu kimeelezwa. Aidha kumejadiliwa yaliyoandikwa kuhusu njeo na halinjeo katika lugha za Kibantu na lugha ya Kingoni. Vilevile, mbinu za utafiti zimebainishwa. Sura ya pili imechunguza vipengele vya fonolojia na mofolojia hususani katika vitenzi vya Kingoni kwa kuzingatia vipengele ambavyo vinahusiana na muundo wa njeo na halinjeo. Sura ya tatu imechanganua mofimu ya njeo katika vitenzi vya Kingoni. Uchanganuzi huo umehusisha viambishi awali, fuatishi, tamati na toni katika kubainisha mofimu hiyo. Sura ya nne imechanganua namna mofimu ya halinjeo inavyoundwa ambapo viambishi na toni pamoja na mazingira ya matukio katika kuundwa kwa halinjeo yameweza kubainishwa. Sura ya tano imehitimisha utafiti huu kwa kutoa muhtasari, matokeo, mapendekezo na changamato za utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yamedhihirisha kuwa kuna viambishi awali, fuatishi na tamati vya njeo katika vitenzi vya Kingoni. Aidha viambishi hasa viambishi awali vya wakati ndivyo vinavyohusika kubainisha halinjeo kwa kushirikiana na viambishi vya matukio. Matokeo hayo pia yamedhihirisha kuwa torn inahusika kubainisha njeo na halinjeo kwa kushirikiana na viambishi vya mofimu hizo. Utafiti huu licha ya kuwezesha kufahamu njeo na halinjeo katika lugha ya Kingoni, pia unaongeza ujuzi wa kiisimu kuhusu njeo na halinjeo katika lugha za Kibantu ikizingatiwa kuwa lugha hii ni miongoni mwa familia ya lugha hizo.
dc.description.sponsorshipKenyatta Universityen_US
dc.identifier.urihttp://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/8082
dc.language.isoKiswahilien_US
dc.titleMuundo wa Njeo Katika Lugha ya Kingonien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Muundo wa Njeo katika Lugha ya Kingoni.pdf
Size:
97.02 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full Text
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: