Upokezi wa Taswira za Matangazo ya Biashara katika Runinga: Kata Ndogo za Nyali na Likoni Kaunti ya Mombasa, Kenya

dc.contributor.advisorKing'ei, Kitula Osore, Miriam
dc.contributor.authorOmuhonja, Elizabeth Nipher
dc.date.accessioned2025-08-01T08:58:43Z
dc.date.available2025-08-01T08:58:43Z
dc.date.issued2025-06
dc.descriptionTasnifu hii Imetolewa ili Kutosheleza baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Juni 2025. Msimamizi Beth Mutugu
dc.description.abstractUtafiti huu ulichunguza upokezi wa taswira za matangazo ya biashara katika runinga. Matangazo kumi ya biashara yanayotangazwa kwa lugha ya Kiswahili yalichunguzwa pamoja na yale ambayo yanachanganya Kiswahili na lugha nyingine. Malengo ya utafiti huu yalikuwa ni kubainisha taswira zinazotumika kwenye matangazo yanayohusu bidhaa za nyumbani katika runinga, kuchanganua taswira zinazotumika kwenye matangazo yanayohusu huduma za mawasiliano katika runinga na kutathmini fasiri za watazamaji kuhusu taswira mbalimbali zilizoteuliwa kwa kuzingatia umri, jinsia na elimu. Sababu ya kufanya utafiti huu ni kuwa swala la kuonyesha namna mbinu ya taswira inavyotumika katika matangazo ya biashara kwa madhumuni ya kuathiri upokezi wa bidhaa zinazotangazwa halijachunguzwa kwa kina. Kazi hii iliongozwa na nadharia mbili; nadharia ya semiotiki iliyoasisiwa na Barthes (1984) inayohusu uhakiki wa ishara na nadharia ya ya upokezi iliyoasisiwa na Iser (1974) inayosisitiza nguvu za mpokeaji au msomaji katika kufasiri kazi anayoipokea na hutilia maanani dhima yake kwa kazi hiyo. Uchunguzi ulifanyika maktabani na nyanjani. Maktabani usomaji wa vitabu, tasnifu, makala na majarida yanayohusu mada ulifanyika kwa kina. Nyanjani data kuhusu fasiri mbalimbali za taswira ilikusanywa kwa kutumia hojaji katika maeneo ya Nyali na Likoni ili kuzitathmini. Matokeo ya utafiti yametolewa kwa njia ya kimaelezo na majedwali. Matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa watangazaji wa matangazo ya biashara hutumia taswira kwa wingi katika matangazo hayo ili kupitisha ujumbe kwa hadhira. Taswira zinazotumika haswa za ishara huhitaji umakinifu wa hali ya juu kutoka kwa hadhira ili waweze kuzifasiri vyema. Taswira za ishara zilipata fasiri mbalimbali kutoka kwa hadhira kwa kuzingatia vigezo vya, umri, jinsia na kiwango cha elimu. Matokeo ya utafiti huu yamewasilishwa katika sura tano. Utafiti huu umetoa mchango kwa wasomi na watafiti kwa kuonyesha namna mbinu ya taswira inavyotumika katika matangazo ya biashara kwa lengo la kuathiri upokezi wake.
dc.description.sponsorshipKenyatta University
dc.identifier.urihttps://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/31005
dc.language.isoen
dc.publisherKenyatta University
dc.titleUpokezi wa Taswira za Matangazo ya Biashara katika Runinga: Kata Ndogo za Nyali na Likoni Kaunti ya Mombasa, Kenya
dc.typeThesis
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Full-text Project.pdf
Size:
3.93 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Tasnifu hii Imetolewa ili Kutosheleza baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Kenyatta, Juni 2025. Msimamizi Beth Mutugu
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
Name:
license.txt
Size:
2.66 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: