Taharuki na Sadfa katika Ujenzi wa Maudhui katika Riwaya za Mwana B’a Yungi Hulewa na Tutarudi na Roho Zetu

Loading...
Thumbnail Image
Date
2022-06
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Kenyatta University
Abstract
Utafiti huu ulishughulikia matumizi ya taharuki na sadfa katika ujenzi wa maudhui katika riwaya za Mwana wa Yungi Hulewa (1976) na Tutarudi na Roho Zetu (1987) zilizoandikwa na Muhammed Said Abdulla na Ben Mtobwa mtawalia. Utafiti huu ulikusudia kuchunguza namna taharuki na sadfa zimetumika kujenga maudhui ya riwaya teule. Malengo ya utafiti yalikuwa kubainisha aina za taharuki zilizotumika katika riwaya teule, kuchanganua aina za sadfa zilizotumika katika riwaya teule na maudhui yaliyojengwa katika riwaya za Mwana wa Mwana wa Yungi Hulewa (1976) na Tularudi na Roho Zetu (1987). Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya uhakiki wa kimtindo kwa mujibu wa Leech (1969). Nadharia ya uhakiki wa kimtindo huchunguza namna mtindo hutumiwa na mtunzi katika kujenga maudhui. Katika utafiti huu, mbinu kusudio iliturnika kuteua aina za taharuki na aina za sadfa zilizotumiwa katika riwaya teule. Aidha, maudhui yaliyojengwa katika riwaya teule yaliangaziwa. Data iliyochanganuliwa ilipatikana kwa kusoma riwaya teule. Data hii ilichanganuliwa kwa kuzingatia mihimili ya nadharia ya uhakiki wa kimtindo kwa kuainisha na kuchanganuaaina za taharuki na aina za sadfa zilizotumika na matokeo kuwasilishwa kwa njia ya maelezo. Uchunguzi huu ulibainisha kuwa: taharuki na sadfa ni muhimu katika kujenga maudhui ya riwaya za kipelelezi, taharuki hutanguliza maudhui yanayoandikiwa na huibua masuala halisi katika jamiina sadfa hupelekea riwaya za kipelelezi kiafikia kilele chake. Utafiti huu ni muhimu kwa kuwa utasgidia wanaosoma kuelewa kuwa taharuki na sadfa huweza kuainishwa kwa mujibu wa wataalamu mbalimbali. Aidha uchunguzi buu utasaidia kufahamu namna taharuki na sadfa zimetumika kujenga maudhui katika riwaya za kipelelezi
Description
Tasnifu Hii Imewasilishwa katika Idara ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Kenyatta kwa Minajili ya Kutosheleza Baadhi ya Mahitaji ya Shahada ya Uzamili, Juni 2022. Wasimamizi 1. Dkt. Miriam Kenyani Osore 2. Dkt. David Kihara
Keywords
Citation