Utomilisi wa Lugha Kama Chanzo cha Ubadilishanaji Msimbo Miongoni mwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Katika Kaunti ya Kiambu
Loading...
Date
2022
Authors
Mwai, Beatrice Njambi
Chacha, Leonard
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
East African Nature and Science Organization
Abstract
Utafiti huu ulichunguza swala la kubadili msimbo miongoni mwa wanafunzi
wa vyuo vikuu Kaunti ya Kiambu. Fikra kuu iliyoongoza utafiti huu ni kuwa
wanafunzi hao hubadili msimbo kwa sababu ya utomilisi wa lugha. Hawana
umilisi mkamilifu wa lugha moja. Kwa mfano, utafiti huu umeangazia lugha
za Kiingereza na Kiswahili. Tumedhihirisha kuwa hawa ni wanafunzi wa chuo
kikuu lakini hawawezi kuwasiliana kwa lugha moja kwa ufasaha, lazima
waingie katika lugha nyingine ili kufanikisha mawasiliano. Kwa mfano, kama
wanatumia lugha ya Kiswahili wanabadilisha na kuingia katika lugha ya
Kiingereza kwa sababu wameshindwa kuendeleza mazungumzo katika lugha
ya Kiswahili. Utafiti huu umeongozwa na nadharia tambulishi
iliyopendekezwa na Myers-Scotton (1983). Kulingana na Myers-Scotton,
katika mawasiliano yoyote, kuna hali ya alama inayotambulika na
isiyotambulika. Katika kuchagua alama, mzungumzaji huchagua alama
kulingana na mahitaji ya kijamii. Pia huonyesha kuwa kubadili msimbo ni kwa
sababu ya ugumu wa watu kutumia lugha moja na ugumu huo uko akilini mwa
mzungumzaji. Utafiti huu umeegemea maktabani na nyanjani. Maktabani,
utafiti huu umenufaika kwa kupata data kutoka kwa machapisho, vitabu na
majarida kuhusu dhana ya kubadili msimbo, uwili lugha na misingi ya
nadharia. Nyanjani, utafiti huu umefanywa katika Kaunti ya Kiambu, Chuo
Kikuu cha Kenyatta na Chuo Kikuu cha Mount Kenya. Utafiti huu umehusisha
matumizi ya vifaa kama vile mwongozo wa mahojiano na kuhudhuria vikao
rasmi ambavyo vijana wanawasiliana. Data iliyochanganuliwa kwa mujibu wa
nadharia tambulishi imewasilishwa kwa njia ya maelezo
Description
Article
Keywords
Kubadili msimbo, Umilisi wa Lugha, Utomilisi wa Lugha, Wingi Lugha
Citation
Mwai, B. N., & Chacha, L. (2022). Utomilisi wa Lugha kama Chanzo cha Ubadilishanaji Msimbo Miongoni mwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu katika Kaunti ya Kiambu. Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 5(1), 64-72.