Uwiano wa picha na matini katika mabango ya matangazo ya ukimwi: mtazamo wa kisemiotiki
dc.contributor.author | Kimani, Hellen Wanjiku | |
dc.date.accessioned | 2011-12-08T08:20:47Z | |
dc.date.available | 2011-12-08T08:20:47Z | |
dc.date.issued | 2011-12-08 | |
dc.description | The PL 8702.K52 | en_US |
dc.description.abstract | Lengo la kazi hii ni kuchanganua uwiano wa maana za picha na matini katika mabango ya matangazo ya UKIMWI kwa kuzingatia tathmini za wapokezi. Watafitiwa ambao walishirikishwa katika utafiti huu waliteuliwa kutoka maeneo ya Githurai na Kiandutu katika wilaya ya Thika. Vitengo vya watu wenye umri, kazi, elimu, tajriba, falsafa na mielekeo tofauti vilihusika. Kwa kurejelea misimbo ya nadharia ya Semiotiki kwa mujibu wa Barthes uchanganuzi wa ishara zote za kisanaa na kiisimu katika mabango thelathini na matano yanayohusu ugonjwa hatari wa UKIMWI yamechanganuliwa. Kazi hii imegawanyika katika sehemu tano. Sura ya kwanza imetanguliza kazi yote kwa kuangazia mada ya utafiti, maswali, malengo, upeo na mipaka ya utafiti. Mengine yaliyoshughulikiwa katika sura hii ni misingi ya nadharia, tahakiki za maandishi yanayohusiana na mada hii, ukusanyaji na uwasilishaji wa data. Sura ya pili imeshughulikia viunzi vya matangazo kwa nia ya kupata maana msingi katika mabango ya UKIMWI, kwa kutalii yale yanayojidhihirisha wazi pasi kuhusisha tajriba, mielekeo na falsafa za mtu binafsi na za kijamii. Sura ya tatu, imeangazia ujumbe katika mabango ya matangazo ya UKIMWI pamoja na kuhakiki dhamira za miguso tofauti. Uhakiki huo uliegemea upande wa yaliyomo kwenye tangazo kama vile: mada, maudhui, wahusika, pamoja na msuko wa picha na matini kwa kurejelea maoni ya watafitiwa. Kwenye sura ya nne, vigezo vya uwiano wa maana na ujumbe katika picha na matini vimeshughulikiwa. Tumechunguza namna picha na matini zinavyohimiliana, kutegemeana na kuathiriana katika kumwelekeza mpokezi kufasiri maana na ujumbe. Tumeangazia pia mchango wa usanii wa picha na matumizi ya lugha kwenye matini katika kufanikisha uwiano wa maana na ujumbe unaofikia hadhira. Sura ya tano imetoa muhtasari wa kazi yote. Aidha, sura hii imeshughulikia matokeo, mahitimisho pamoja na mapendekezo ya utafiti wa baadaye kwa azima ya upanuzi wa mawasiliano ya ishara za kisanaa katika hatua za kuboresha uwasilishaji wa maana na ujumbe, ili yaende sambamba na yale ya ishara za kiisimu. | en_US |
dc.description.sponsorship | Kenyatta University | en_US |
dc.identifier.uri | http://ir-library.ku.ac.ke/handle/123456789/1935 | |
dc.language.iso | en | en_US |
dc.subject | Swahili language--Grammar//AIDS(Disease) and mass media//AIDS(Disease) in mass media//Semiotics//Visual communication | en_US |
dc.title | Uwiano wa picha na matini katika mabango ya matangazo ya ukimwi: mtazamo wa kisemiotiki | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |
Files
Original bundle
1 - 1 of 1
Loading...
- Name:
- Uwiano wa picha na matini katika mabango ya matangazo ya ukimwi mtazamo wa.pdf
- Size:
- 97.59 MB
- Format:
- Adobe Portable Document Format
- Description:
- Thesis full text
License bundle
1 - 1 of 1
No Thumbnail Available
- Name:
- license.txt
- Size:
- 2.68 KB
- Format:
- Item-specific license agreed upon to submission
- Description: